Pata taarifa kuu
BRAZILI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Brazil yashikilia nafasi ya pili kwa vifo zaidi duniani

Tangu Ijumaa wiki hii Brazil inaendelea kushikilia nafasi ya pili kwa vifo zaidi duniani vinavyohusiana na janga la Covid-19 baada ya Marekani ambayo inaongoza kwa visa zaidi ya Milioni 2 vya maambukizi.

Brazili yaendelea kukumbwa na Corona.
Brazili yaendelea kukumbwa na Corona. REUTERS/Amanda Perobelli
Matangazo ya kibiashara

Brazil ambayo kufikia sasa imerekodi vifo 41,828 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo, inaongoza mbele ya Uingereza kwa idadi kubwa ya vifo kutokana na Corona.

Brazil, ambayo ni nchi kubwa katika ukanda wa Amerika ya Kusini (yenyeji wakaazi milioni 212) pia ni ya pili kwa idadi kubwa ya maambukizi yaliyothibitishwa nyuma ya Marekani, ikiwa na visa 828,810 vya maambukizi, shirika la habari la AFP limeripoti.

Kufikia sasa wagonjwa 397,000 wamepona na watu 41,828 wamefariki dunia kutoka na ugonjwa huo hatari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.