Pata taarifa kuu
BRAZILI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Jair Bolsonaro atishia kuiondoa Brazili kwenye unachama wa WHO

Rais wa Brazili Jair Bolsonaro ametangaza kwamba anafikiria kuiondoa Brazil kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa sababu ya "upendeleo wa kiitikadi" katika mgogoro wa afya unaosababishwa na virusi vya Corona.

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro akiwa barakoa katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano Machi 18 huko Brasilia.
Rais wa Brazil Jair Bolsonaro akiwa barakoa katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano Machi 18 huko Brasilia. Sergio LIMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya Donald Trump, sasa ni zamu ya rais wa Brazil Jair Bolsonaro kutishia kuindoa nchi yake kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Baada ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa kuonya serikali za Amerika kusini juu ya hatari itakayotokana na kulegeza kwa masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona kabla ya kupunguza kusambaa kwa janga la Corona katika ukanda huo, rais wa Brazil alionya jana Ijumaa kwamba anaweza kuiondoa nchi yake kwenye uanachama wa WHO kupinga dhidi ya "upendeleo" wa kiitikadi.

"Ninawaambia hapa, Marekani imejiondoa kwenye uanachama wa WHO, tunafikiri na sisi kufanya hivyo katika siku zijazo (...). Aidha WHO ifanye kazi bila upendeleo wa kiitikadi, au pia tujiondoe kwenye uanachama wa shirika hilo, " amesema rais Bolsonaro.

“Hatuitaji watu wa nje kutoa hisia zao juu ya afya hapa," Bolsonaro aliwaambia waandishi wa habari huko Brasilia.

Katika wakati wote wBrazili ilipokuwa ikikumbwa na mgogoro wa afya, Bolsonaro alijitahidi kuiga mwenendo wa Trump kwa kupuuzia hatari ya ugonjwa huo, akiwataka raia wake kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kawaida bila kujilinda, na kusifu ufanisi wa dawa ya hydroxychloroquine ambayo imewagawa wanasayansi.

Akiongea juu ya mada hiyo, rais huyo wa Brazil alisema hajashangaa kuwa utafiti katika jarida la matibabu la Lancet, ambao lilihitimisha kuwa dawa hiyo haina maana, na kutiliwa mashaka na kisha kufutwa. Hali hiyo ililisababisha WHO kuanza tena majaribio ya kliniki kuhusu dawa hiyo.

Siku ya Alhamisi, vifo vipya viliiweka Brazil mbele ya Italia kwa idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na Corona.

Wakati huo huo Bolsonaro anaendelea kuomba nchi yake iondolewe haraka vikwazo, akisema kwamba mdororo wa kiuchumi uliosababishwa na janga hilo unazidi hatari ya afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.