Pata taarifa kuu
MAREKANI-ICC-HAKi-USALAMA

Marekani yatangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya maafisa wa ICC

Rais wa Marekani ameidhinisha vikwazo vya kiuchumi na marufuku ya kusafiri nchini Marekani dhidi ya maafisa wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai na maafisa wanaohusika katika faili za Afghanistan na Palestina, zilizofunguliwa na mwendesha mashtaka Fatou Bensouda.

Rais Donald Trump katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White Mei 26, 2020.
Rais Donald Trump katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White Mei 26, 2020. Win McNamee/Getty Images/AFP
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivi pia vinalenga familia zao na watu wao wa karibu. Tangazo hilo limetangazwa na Waziri wa Mambo ya nje Mike Pompeo.

"Hatuwezi kukaa kimya wakati watu wetu wanatishiwa na mahakama isiyofaa - na hatutokubali," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amesema.

"Kwanza, tunatoa idhini ya kuchukuliwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya maafisa wa ICC wanaohusika moja kwa moja katika uchunguzi wa maafisa wa Marekani na washirika wake bila idhini ya nchi hizo, na dhidi ya wale ambao wanaunga mkono kifedha shughuli hizo za uchunguzi. Vikwazo vitachukuliwa kesi kwa kesi dhidi ya watu au nchi maalum. "

"Pili, Marekani haitokubali kutoa visa zake kwa wale wanaohusika moja kwa moja katika uchunguzi huo, na vikwazo hivyo pia vitachukuliwa dhidi ya familia zao," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameongeza. Hii haitupi furaha kuwaadhibu. Lakini hatuwezi kuruhusu maafisa wa ICC na familia zao kuja Marekani kula, kusafiri, kwa maneno mengine kunufaika na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujiskia huru nchini Marekani wakati watu hao wanataka kuwashtaki wale wanaotetea uhuru huo. "

Vitisho vya utawala wa Trump vimekuepo dhidi ya Mahakama hiyo ya kimataifa tangu mwaka wa 2018. Hata hivyo vitisho hivyo havijazuia uchunguzi kuhusu uhalifu uliofanywa na jeshi la Marekani na shirika la ujasusi la CIA nchini Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.