Pata taarifa kuu
CANADA-MAUAJI-USALAMA

Canada yaomboleza vifo vya raia wake 18

Uchunguzi unaendelea nchini Canada kujua jinsi gani mauaji makubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni ya nchi hiyo yametokea na kwanini mtu mwenye umri wa miaka 51aliauwa watu wasiopungua 18 kabla ya kupigwa risasi na polisi.

Watu kumi na sita akiwemo afisa wa polisi mwanamke waliuawa katika shambulio la risasi katika kijiji kidogo cha Portapique, huko Nouvelle-Écosse, Mashariki mwa Canada.
Watu kumi na sita akiwemo afisa wa polisi mwanamke waliuawa katika shambulio la risasi katika kijiji kidogo cha Portapique, huko Nouvelle-Écosse, Mashariki mwa Canada. REUTERS/John Morris
Matangazo ya kibiashara

Wachunguzi kutoka kikosicha Polisi ncini Canada wanajaribu kujua kilichosababisha Gabriel Wortman, daktari wa meno, mwenye umri wa miaka 51, ambaye hjawahi kuwa na makosa ya jinai katika miaka ya nyuma, aliweza kutekeleza kitendo hicho kiovu.

Hata hivyo inasemekana kuwa uchunguzi huo unaonekana utachukuwa muda mrefu.

Kwa jumla, si chini ya matukio kumi na sita ya uhalifu yaliyothibitishwa nchini Canada. Na idadi ya vifo - kumi na nane - inaweza kuongezeka zaidi katika siku zijazo, kwani wachunguzi wana hofu ya kupata miili mingine zaidi chini ya vifusi vya nyumba ambazo mtuhumiwa aliteketeza kwa moto, ameripoti mwandishi wetu wa Quebec, Pascale Guéricolas.

Uchunguzi ambao unaonekana kuwa tata unaweza kudumu "miezi kadhaa", ameisema Chris Leather, mkuu wa polisi nchini Canada (GRC).

Mauaji hayo yalitokea katika kijiji kidogo cha Portapique, huko Nouvelle-Ecosse, mashariki mwa Canada, karibu na bahari ambapo muuaji mwenye umri wa miaka 51anamiliki nyumba kadhaa. Baada ya kuuwa watu kadhaa anaowajua, alifanikiwa kutoroka, kwa mujibu wa afisa wa anafanya uchunguzi, akitumia gari linalofanana na la polisi ya nchi hiyo. hata hivyo aliuawa baada katika makabiliano ya urushianaji risasi yaliyodumu saa kumi na mbili na polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.