Pata taarifa kuu
CANADA-MAUAJi-USALAMA

Canada: Watu 16 wauawa katika shambulio la risasi Nouvelle-Écosse

Watu kumi na sita akiwemo afisa wa polisi mwanamke wameuawa katika shambulio la risasi lililoendeshwa na mtu mwenye silaha katika kijiji kidogo cha Nouvelle-Écosse, Mashariki mwa Canada, kabla ya kudhibitiwa na polisi.

Shambulio hilo lilianziahuko Portapique, Nouvelle-Ecosse, ambapo watu kadhaa waliuawa Jumamosi Aprili 18.
Shambulio hilo lilianziahuko Portapique, Nouvelle-Ecosse, ambapo watu kadhaa waliuawa Jumamosi Aprili 18. REUTERS/John Morris
Matangazo ya kibiashara

Haya ni mauaji mabaya kuwahi kutoka nchini Canada tangu miaka thelathini iliyopita.

Kwa muda wa saa 12 za makabiliano, polisi polisi ilizingira kituo cha mafuta, na mshambuliaji anadaiwa kuwa ameuawa, huku shambulio la muuaji huyo likigharimu maisha ya watu 16; kulingana na ripoti ya awali. Afisa wa polisi mwanamke mwenye miaka 23 ya uzoefu ni miongoni mwa watu waliouawa.

Shambulio hilo lilianza Jumamosi na kumalizika Jumapili huko Nouvelle-Écosse, Mashariki mwa Canada. Sababu za mshambuliaji Gabriel Wortman, 51, kutekeleza shambulio hilo hazijajulikana bado, lakini uchunguzi wa kina utahitajika kabla ya kuelewa mazingira ya uhalifu huo uliofanywa, ameripoti mwandishi wetu, Pascale Guéricolas.

Wahanga kadhaa waligunduliwa mbele na ndani ya nyumba inayomilikiwa na mshambuliaji, ambapo polisi waliitwa baada ya kusikika milio ya risasi.

Mshambuliaji alitumia gari linalofanana na magari ya polisi baada ya askari polisi kuzingira nyumba yake, kwa mujibu wa mashahidi.

"Operesheni imemalizika leo asubuhi wakati mtuhumiwa aligunduliwa alikojificha. Naweza kudhibitisha kwamba ameuawa, "afisa wa polisi wa maswala ya upelelezi kuhusu makosa ya jinai katika kijiji cha Nouvelle-Écosse, Chris Leather amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.