Chama cha Justin Trudeau chashinda uchaguzi Mkuu Canada
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ameshinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana na kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili, kwa mujibu wa matokeo ya awali.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Televisheni ta Taifa CBC inabashiri kuwa, chama cha Liberal cha Waziri Mkuu Trudeau kinaelekea kupata ushindi, na hivyo kitaunda serikali, lakini hakitakuwa na idadi kubwa mno ya viti bungeni.
Tayari wafuasi wa chama hicho wameanza kusherehekea ushindi huo jijini Montreal, wakati huu wakisubiri hotunba kutoka kwa kiongozi wao.
Hata hivyo, wafuasi wa chama cha Conservative kinachoongozwa na Andrew Scheer ambaye ameleta ushindani mkubwa, wameonekana wenye huzuni, baada ya kubainika kuwa watapoteza katika Uchaguzi huu.
Mamilioni ya raia wa Canada walishiriki katika Uchaguzi huu, ulioshuhudia idadi kubwa ya wanawake wakiwania nyadhifa ya kuwa Waziri Mkuu.