Pata taarifa kuu
VENEZUELA-COLOMBIA-USALAMA

Maduro aituhumu Colombia kutaka kuzua migogoro na Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameishtumu mwenzake wa Colombia Ivan Duque "kufanya kilio chini ya uwezo wake" ili "kuzua mgogoro" kwa kisingizio kwamba viongozi wa zamani wa waasi wa FARC wameamua kurudi kushika silaha.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro (Kushoto) akiwa pamoja na maafisa wa jeshi la Venezuela.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro (Kushoto) akiwa pamoja na maafisa wa jeshi la Venezuela. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inaonyesha mvutano mpya katika uhusiano ambao tayari umeingiliwa na dosari baina ya viongozi hao wawili.

Mbele ya askari waliokusanyika kwa sherehe mjini Caracas, Rais wa Venezuela amemshtumu Ivan Duque kwa kutumia "madai yasiyokuwa na msingi kushambulia kimaneno Venezuela na kuzua mgogoro wa kijeshi dhidi ya nchi yetu". Rais Maduro amesema Bogota imesema inatumia maneno hayo makali "kukazia" shutuma hizi na kuzidisha mivutano.

Wanajeshi waliopelekwa kando ya mpaka unaogawa nchi hizi mbili, kwenye umbali wa kilomita 2,200, wamewekwa kwenye "tahadhari ya kiwango cha juu (...) kwa tishio la uchokozi wa Colombia dhidi ya Venezuela," ametangaza Nicolas Maduro bila hata hivyo kufafanua kinachomaanisha "tahadhari ya kiwango cha juu".

Uhusiano kati ya rais wa kisoshalisti na mwenzake wa mrengo wa kulia Ivan Duque tayari umeingiliwa na dosari. Lakini vita vya maneno kati ya wakuu wa nchi hizi mbili viliongezeka wiki iliyopita kuhusu wapiganaji wenye silaha kutoka Colombia ambao kwa mujibu wa Rais Ivan Duque, "wanapewa hifadhi" na "kusaidiwa" na serikali ya Venezuela. Tuhuma hizi zilitolewa wakati waasi wa zamani wa FARC kutoka Colombia, walikataa makubaliano ya kihistoria ya amani ya mwaka 2016 na kutangaza kwamba watarudi kushika silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.