Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MAZUNGUMZO-USALAMA-SIASA

Mazungumzo kati ya serikali na upinzani kuanza tena Venezuela

Mwanasiasa wa upinzani Juan Guaidó, anayetambuliwa kama rais wa mpito na zaidi ya nchi hamsini, ametangaza siku ya Jumapili Julai 7, kuanza tena kwa mazungumzo wiki hii, huko Barbados, chini ya shinikizo la Norway.

Juan Guaidó, aliyjitangaza rais wa mpito wa Venezuela, wakati wa maandamano, Caracas Julai 5, 2019.
Juan Guaidó, aliyjitangaza rais wa mpito wa Venezuela, wakati wa maandamano, Caracas Julai 5, 2019. REUTERS/Manaure Quintero
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa upinzani, tangazo la kuanza tena kwa mazungumzo linaonekana kama dalili za kushindwa. Mapema mwezi Julai, ilikuwa haiwezekani kwa Juan Guaidó kukubali mazungumzo kwa sababu ya kifo cha askari aliyekuwa kizuizini, ambaye inadhaniwa kuwa aliuawa kwa mateso. Kwa leo, Juan Guaidó anamuunga mkono Nicolas Maduro ambaye amekuwa akisema kwa wiki kadhaa kwamba mazungumzo yanatarajia kuanza tena.

Kwa leo inaonekana kwamba kiongozi wa upinzani amejibamiza kwenye ukuta, hana njia nyingine ya kutumia. Wito wake wa maandamano hauitikiwi tena na shinikizo la kimataifa linaonekana kuwa halina athari kwa mpinzani wake, ambaye anaendelea kusalia mamlakani. Hata vikwazo vya Marekani havimtikisi, isipokuwa kuongeza maisha duni kila kukicha kwa raia wa Venezuela ambao wamechoshwa na ahadi zisizokuwa na matokeo.

Kutokana na hali hii, upinzani umebakiliwa na njia mbili tu. Moja, ya msimamo mkali, wa kuomba nchi yao kuingiliwa kijeshi kwa masaada wa majeshi kutoka nje. Jambo ambalo haliwezekani, licha ya kuwa bado linafikiriwa sana. Juan Guaidó pia ametangaza siku ya Jumapili kuwa Venezuela iitajiunga na TIAR, mkataba wa ushirikiano wa kijeshi katika bara la Amerika.

Njia ya pili, ni mazungumzo ya amani, na ya kweli. Lakini mara nyingine tena, upinzani unaonekana kuwa na msimamo wa kutaka rais Nicolas Maduro aondoke mamlakani. Na hivyo ndivyo vilivyofanya mazungumzo ya kwanza kushindwa huko Oslo mnamo mwezi Mei.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.