Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

James Mattis: Lengo la Washington si vita

Lengo la Marekani "sio vita" na Korea Kaskazini, amesema Ijumaa hii Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis alipokua akizuru eneo la mpakani linalotenganisha Korea Kaskazini na Korea Kusini.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis (katikati) anaongea na waandishi wa habari, pamoja na mwenzake wa Korea Kusini Song Young-Moo (kulia),  Panmunjom katika eneo la  mpakani linalotenganisha Korea mbili (DMZ), Oktoba 27, 2017.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis (katikati) anaongea na waandishi wa habari, pamoja na mwenzake wa Korea Kusini Song Young-Moo (kulia), Panmunjom katika eneo la mpakani linalotenganisha Korea mbili (DMZ), Oktoba 27, 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hali ya sintofahamu imeendelea kushuhudiwa kwenye rasi ya Korea tangu mapema mwaka 2016, na hasa katika miezi ya hivi karibuni.

Hii ni kutokana na kasi ya mipango ya nyuklia na makombora ya masafa marefu ya Pyongyang, ambayo ilifanyajaribio la sita la nyuklia mapema mwezi Septemba. Na kwa upande mwingine, kauli za vita zimekua zikitolewa kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un na Rais wa Marekani Donald Trump , ambaye mnamo mwezi Novemba atazuru Korea Kusini.

Lakini Bw. Mattis, ambaye alizuru eneo la mpakani kati linalotenganisha Korea mbili (DMZ), amsema Ijumaa hii kuwa Marekani imeku ikitaka "ufumbuzi wa kidiplomasia."

"Kama alivyosem aWaziri wa Mashauriano ya Kigeni Rex Tillerson, lengo letu sio vita lakini badala ya kuachana na mpango wa nyuklia kikamilifu, katika rasi ya Korea," amesema katika kijiji cha mpakani cha Panmunjom.

Amesema kuwa mwenzake wa Korea Kusini, Song Young-Moo na yeye "wamehakikishia kujitolea kwa pamoja kwa ufumbuzi wa kidiplomasia ili kukabiliana na tabia isiyo nzuri ambayo ni kinyume na sheria ya Korea Kaskazini."

James Mattis na Song Young-Moon watashiriki katika mkutano wa kila mwaka wa masuala ya ulizi siku ya Jumamosi Oktoba 28.

Rais Donald Trump atazuru Korea ya Kusini tarehe 7 na 8 Novemba. Na hotuba yake inasubiri kwa hamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.