Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-AUSTRALIA-MAREKANI-USALAMA

Korea Kaskazini yaionya Australia kutokuwa na ushirikiano na Marekani

Korea Kaskazini kupitia barua iliyotumwa kwa viongozi wa Australia imeionya nchi hiyo kutothubutu kushirikiana na Marekani, ambayo kwa mujibu wa serikali ya Korea Kaskazini, imetangaza kuingamiza Korea Kaskazini iwapo italazimika kujilinda.

Kiongozi wa JKorea Kaskazini Kim Jong-un.
Kiongozi wa JKorea Kaskazini Kim Jong-un. Ed JONES / AFP
Matangazo ya kibiashara

Barua hiyo yenye ukurasa mmoja ilitumwa kupitia ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Indonesia na inadaiwa kutoka kwa kamati ya maswala ya kigeni ya Korea Kaskazini.

Serikali ya Australia imesema kuwa imepokea barua kutoka Korea Kaskazini ikiitaka kutojihusisha na utawala wa rais Trump.

Maafisa waandamizi wa Aaustralia wamesema kuwa barua hiyo pia ilitumwa kwa mataifa mengine.

Waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull amesema barua hiyo inaonyesha kuwa shinikizo za kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskzini zimeanza kufanya kazi, licha ya kuonekana kutojali umuhimu wa barua hiyo.

Korea Kaskazini kupitia barua hiyo imezitaka serikali nyengine kujitenga na hatua zisizokuwa na heshima za rais Trump ikisisitiza kuwa Marekani inaweza kusababisha janga kubwa la kinyuklia.

Bwana Turnbull amesema kuwa Korea Kaskazini ndio inayosababisha wasiwasi kwa kutishia kuyashambulia mataifa ya Japan, Korea Kusini na Marekani kwa kutumia silaha za kinyuklia.

Vita vya maneno vimekua vikiendelea kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongzi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Viongozi wa Australia wanakubaliana kwamba huenda ni ishara kwamba shinikizo za kimataifa dhidi ya Korea Kaskazini zimeanza kuzaa matunda na kuwa na matumaini kwamba kutakuwa na majadiliano ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.