Pata taarifa kuu
MAREKANI-VENEZUELA-VIKWAZO

Marekani yawachukulia vikwazo maafisa kadhaa nchini Venezuela

Serikali ya Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo maafisa 13 wa vyeo vya juu nchini Venezuela wakati ambapo rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro akiendelea kukabiliwa na shinikizo zaidi. Uchaguzi wa bunge jipya la kubuni katika mpya unaokumbwa na utata, umepangwa kufanyika siku ya Jumapili Julai 30.

Rais Nicolas Maduro venezuela akipokea hati ya kuidhinisha sheria kwa "mamlaka yake ya kipekee", Novemba 11, 2013.
Rais Nicolas Maduro venezuela akipokea hati ya kuidhinisha sheria kwa "mamlaka yake ya kipekee", Novemba 11, 2013. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, Rais Donald Trump aliapa kuchukua hatua kali za kiuchumi ikiwa Bwana Maduri ataandaa kura hiyo ya maoni siku ya Jumapili.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa majeshi ni miongoni mwa maafisa wa ngazi za juu waliolengwa na vikwazo hivyo vya Marekani.

Vikwazo hivyo pia vinamlenga mkuu wa baraza la uchaguzi Tibisay Lucena, aliyekuwa makamu wa rais Elias Jaua ambaye anaongoza tume zinaoandaa uchaguzi wa Jumapili.

Vikwazo hivyo ni vya kutwaliwa mali ya maafisa hao nchini Marekani na kuyazuia makampuni ya Marekani kufanya biashara nao.

Wakati huo huo rais Nicolas Maduro amesema kuwa vikwazo vya Marekani ni kinyume na sheria

Mgomo dhidi ya Katiba mpya ya Maduro waendelea Venezuela

Makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama yalizuka siku ya Jumatano Julai 26 nchini Venezuela, na kusababisha kifo cha mtu mmoja, wakati wa mgomo wa saa 48 uliyoandaliwa na upinzani dhidi ya uchaguzi wa Jumapili wa wabunge watakaosimamia katiba mpya.

Mtu aliyeuawa wakati wa maandamano katikajimbo la Merida (magharibi mwa Venezuela), alikua na umri wa miaka 30. Mahakama imeanzisha uchunguzi. Idadi ya watu ambao wameuawa katika maandamano hayo yaliyoanza miezi minne iliyopita imefikia 103, huku maelfu ya watu wakijeruhiwa na maelfu wengine wakiendelea kushikiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.