Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI

Mtoto wa rais Trump akiri kukutana na wakili kutoka Urusi

Mtoto wa kiume wa rais wa Marekani Donald Trump amekiri kukutana wakili wa Urusi, kipindi cha kampeni za kisiasa mwaka uliopita, baada ya wakili huyo kumwambia kuwa alikuwa na taarufa za kumchafulia jina aliyekuwa mpinzani wa baba yake, Hillary Clinton.

Donald Trump Jr mtoto wa rais Donald Trump
Donald Trump Jr mtoto wa rais Donald Trump REUTERS/Stephanie Keith
Matangazo ya kibiashara

Donald Trump Junior amesema licha ya kutana na wakili huyo, hakupeleka taarifa alizozipata popote.

Ripoti ya mkutano huu, ilitolewa na Gazeti la New York Times na inakuja wakati huu Shirika la FBI na Buneg la Congress likiendelea na uchunguzi kubaini iwapo Urusi iliiingia Uchaguzi wa Marekani na kumsaidia Trump kupata ushindi.

Urusi imesema kuwa haikuwahi kuingilia Uchaguzi wa Marekani, kauli ambayo rais Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter baada ya kukutana na rais Vladimir Putin pembezoni mwa mkutano wa G20 nchini Ujerumani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.