Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Trump: Muda umewadia wa kufanya kazi vilivyo na Urusi

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anataka kufanya kazi kwa karibu na nchi ya Urusi ikiwemo masuala yanayohusu usalama wa kwenye mtandao licha ya mara kadhaa kumkosoa rais Vladimir Putin kuwa nchi yake iliingilia uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema umefika muda kwa uhusiano wa nchi yake na Urusi kusonga mbele.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema umefika muda kwa uhusiano wa nchi yake na Urusi kusonga mbele. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Wakati huu akitangaza kutoondoa vikwazo dhidi ya Urusi kutokana na mzozo wa Urusi na Ukraine, rais Trump amesema umefika muda kwa uhusiano wa nchi yake na Urusi kusonga mbele hata kama baadhi ya wanasiasa ndani ya chama chake wakitaka kuchukuliwa kwa vikwazo zaidi dhidi ya Urusi.

Siku tatu baada ya kukutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza na rais wa Urusi, kando na mkutano wa G20 uliofanyika mwishoni mwa juma nchini Ujerumani, rais Trump amesema alimuhoji rais Putin kuhusu ushahidi kuwa nchi yake iliingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Katika hatua nyingine vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa mtoto wa rais Trump alikubali kukutana na mwanasheria wa serikali ya Urusi mwaka jana baada ya kuahidiwa kupewa taarifa zitakazomchafua aliyekuwa mgombea wa Democrats, Hillary Clinton.

Trump Junior amekiri kukutana na mwanasheria huyo lakini akasisitiza hawakubadilishana taarifa zozote kuhusu mgombea wa Democrats, Hillary Clinton.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.