Pata taarifa kuu
HAITI-MARTELLY-UTEUZI-MAANDAMANO-SIASA

Evans Paul ateuliwa kuwa Waziri mkuu Haiti

Rais wa Haiti, Michel Martelly, amemteua Evans Paul kuwa Waziri mkuu wa Haiti, wiki tatu baada ya Laurent Lamothe, kujiuzulu kwenye wadhifa huo.

Michel Martelly amethibitisha rasmi uteuzi wa Evans Paul, kwa sheria ya kiraisi iliyotolewa jioni ya Alhamisi Desemba 25 mwaka 2014.
Michel Martelly amethibitisha rasmi uteuzi wa Evans Paul, kwa sheria ya kiraisi iliyotolewa jioni ya Alhamisi Desemba 25 mwaka 2014. REUTERS/Hannibal Hanschke/Files
Matangazo ya kibiashara

Laurent Lamothe ni rafiki wa muda mrefu wa rais Michel Martelly. Evans Paul ni kutoka upande wa upinzani ambaye aliwahi kuwa mwandishi wa habari.

Rais wa Haiti amemteua mwandishi huyo wa habari wa zamani kutoka upande wa upinzani ili aweze kupunguza hasira za waandamanaji ambao wamekua wakiandamana kwa majuma kadhaa katika mji wa Port-au-Prince na katika baadhi ya mikoa.

Watu wengi wamekua wakizagaza uvumi tangu siku kadhaa zilizopita kuwa Evans Paul huenda ndiye akateuliwa kwenye wadhifa wa Waziri mkuu. Michel Martelly amethibitisha rasmi uteuzi huo kwa sheria ya kiraisi, iliyotolewa jioni ya Alhamisi Desemba 25 mwaka 2014.

Evans Paul, mwenye umri wa miaka 59 ana ushawishi mkubwa katika jamii ya wanasiasa nchini Haiti. Evans paul, alichaguliwa mwaka 1990 kuwa mkuu wa manispaa ya jiji la Port-au-Prince, lakini hakuweza kutekeleza majukumu yake kutokana na jaribio la mapinduzi lililofanyika mwaka 1991. Hivi karibuni Evans Paul amekua akimkosoa rais Michel Martelly kutokana na uongozi wake, ambao unadaiwa kuwa unawakandamiza wapinzani.

Uteuzi huo wa Evans Paul unatazamiwa kupitishwa na bunge la taifa pamoja na baraza la Seneti.

Hata hivyo wapinzani wenye msimamo mkali hawajaamua kusitisha maandamano yao. Wamepanga kuandamana Jumapili 28, Jumanne Desemba 30 na Alhamisi Januari 1 katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince wakiomba rais Michel Martelly ajiuzulu haraka iwezekanavyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.