Pata taarifa kuu
ARGENTINA-UCHAGUZI-SIASA

Argentina yafunua ukurasa mpya kwa kuchaguliwa kwa Mauricio Macri

Mauricio Macri kutoka chama cha Conservative amechaguliwa Jumapili hii kuwa rais wa Argentina katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais. uchaguzi ambao umeashiria mwisho wa utawala wa Kirchner alieliongoza taifa hilo la tatu kwa uchumi katika eneo la Amerika ya Kusini.

Mauricio Macri katika mji wa Buenos Aires Novemba 22, 2015.
Mauricio Macri katika mji wa Buenos Aires Novemba 22, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kura zote zimehesabiwa na Macri amefanikiwa kupata ushindi wa asilimia 52 mbele ya mpinzani wake Daniel Scioli aliyepata asilimia 48.

Huu ni ushindi wa kwanza wa Conservative nchini humo kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Mauricio Macri, mwenye umri wa miaka 56, amemshinda Daniel Scioli, mgombea wa serikali ya mseto, ambaye alikuwa alipewa nafasi kubwa ya kushinda kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi.

Daniel Scioli akipiga kura katika kata ya Tigre, katika jimbo la Buenos Aires Novemba 22, 2015.
Daniel Scioli akipiga kura katika kata ya Tigre, katika jimbo la Buenos Aires Novemba 22, 2015. JUAN MABROMATA/AFP

Rais Cristina Fernández de Kirchner kutoka chama cha mrengo wa kushoto, anaiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2007 baada ya kumrudilia mume wake, ambaye hakuweza kugombea awamu ya tatu mfululizo, kwa mujibu wa katiba.

Mara tu baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kwanza, wafuasi wa meya wa Buenos Aires, walikutana katika makao makuu ya muungano wa vyama vya upinzani wa Cambiemos (ikimaanisha tubadili) unaongozwa na Macri, wamejipongeza na kuanza kusherehekea ushindi.

Wafuasi wa Mauricio Macri jijini Buenos Aires, Novemba 22, 2015.
Wafuasi wa Mauricio Macri jijini Buenos Aires, Novemba 22, 2015. JUAN MABROMATA/AFP

Mauricio Macri atajitahidi kushirikiana na taasisi zingine za uongozi wa nchi kwa kuliongoza taifa hilo, kwani muungano wake hauna wingi wa viti katika Baraza la wawakili na Baraza la Seneti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.