Pata taarifa kuu
ARGENTINA-UCHAGUZI-SIASA

Argentina: matokeo ya mshangao ya Macri katika duru ya 1

Mgombea wa chama cha mrengo katikati Kushoto, Daniel Scioli, anaye ungwa mkono na rais anayemaliza muda wake Cristina Kirchner, alipewa nafasi ya kushinda katika duru ya kwanza lakini atalazimika kuingia kushindana katika duru ya pili ya uchaguzi na mgombea wa chama cha Conservative, Mauricio Macri.

Mgombea wa chama cha Conservative Mauricio Macri akifurahia matokeo ya uchaguzi Oktoba 25, 2015 katika makao makuu ya chama chake jijini Buenos Aires jioni ya raundi ya kwanza ya uchaguzi wa rais.
Mgombea wa chama cha Conservative Mauricio Macri akifurahia matokeo ya uchaguzi Oktoba 25, 2015 katika makao makuu ya chama chake jijini Buenos Aires jioni ya raundi ya kwanza ya uchaguzi wa rais. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Duru ya pili ya uchaguzi huo itafanyika Novemba 22.

Kura za hivi karibuni zilimpa Mauricio Macri, mwenye umi wa miaka 56, Meya wa mji wa Buenos Aires tangu mwaka 2007, pointi 10 nyuma ya Scioli. Baadhi walitabiri ushindi wa Scioli katika duru ya kwanza.

Baada ya uhasibu wa 90% ya vituo vya kupigia kura, Daniel Scioli amefikia 36.12% ya kura, mbele ya Mauricio Macri kwa 34.97% ya kura.

" Ni mshangao mkubwa kuona wagombea wanashinda kwa asilimia ndogo kiasi hicho. Matokeo haya yameshangaza wengi ”, amebaini mwanasaikolojia Gabriel Puricell.

Enzi mpya nchini Argentina baada ya miaka 12 ya utawala wa Nestor Kirchner (2003-2007) na mke wake Cristina Kirchner (2007-2015), ambaye hangeliweza kuwania awamu ya tatu.

Nchini Argentina, inatosha tu kuwa na 45% ya kura katika duru ya kwanza, au tu 40% ikiwa tofauti na wa pili inafikia pointi 10.

Tangu mwaka 1973, Argentina ilipitisha kanuni ya uchaguzi wa urais kwa duru mbili, lakini chaguzi saba zilizoitishwa tangu mageuzi ziliamuliwa kufuatana na duru ya kwanza.

Mwaka 2003, Nestor Kirchner hakuwa na kura za kutosha ili kuepuka duru ya pili, lakini mshindani mwenza Carlos Menem alijiuzulu kabla pambano hilo

Takriban wananchi Milioni thelathini na mbili kwa jumla ya milioni 41 wametakiwa kupiga muhuri wa sura ya kumi na mbili wa utawala wa Nestor (2003-2007) na Cristina Kirchner (2007-2015). Vituo vya kupigia kura vimefungwa saa 12:00 joni saa za Argentina (sawa na saa 3:00 usiku saa za kimataifa).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.