Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Chad: Mapigano mapya mabaya yazuka kati ya wafugaji wa na wakulima

Takriban watu 23 waliuawa mwishoni mwa mwezi Machi katika siku saba za mapigano kati ya wafugaji na wakulima kusini mwa Chad, ambayo mara kwa mara inakabiliwa na mapigano makali kati ya jamii hizi za kuhamahama na wakulima, Waziri wa Kilimo ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu.

Vurugu kati ya wafugaji na wakulima hutokea mara kwa mara katikati na kusini mwa Chad, ambako wakazi wengi wana silaha.
Vurugu kati ya wafugaji na wakulima hutokea mara kwa mara katikati na kusini mwa Chad, ambako wakazi wengi wana silaha. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yanahusisha jamii mbili, wafugaji wa kuhamahama wa Kiarabu dhidi ya wakulima wa kiasili wasiofanya kazi, Wafugaji wamekuwa wakipitisha  au kuchunga mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima, au kubishana kuhusu umiliki wa baadhi ya ardhi.

Mapigano haya mapya, kufuatia "mauaji" ya mwanamume kutoka jamii ya Waarabu katika shambulio la kuvizia, yalizuka kati ya Machi 21 na 27 katika vijiji vitatu katika eneo la Chari ya Kati - Balwaï, Kolo na Balkoutou - kusini mwa Chad, eneo lenye rutuba, Waziri Abdraman Koulamallah ameliambia shirika la habari la AFP. Wazazi wa muathiriwa na watu wa ukoo wake, ambao wanatoka eneo la kaskazini ambalo ni kame na mifugo yao, waliongoza msafara wa katika kijiji cha jamii ya wakulima wa Sara-Kaba, ambao waliwatuhumu kwa kufanya shambulio la kuvizia, kulingana na waziri ambaye amehakikishia Jumatatu kwamba utulivu umerejea.

Mapigano hayo, ambayo yaliendelea kwa siku saba katika vijiji vingine viwili, yalisababisha jumla ya watu tisa kuuawa miongoni mwa jamii ya Waarabu na 14 kati ya jamii ya wakulima ya Sara-Kaba, wakiwemo wanawake wanne na watoto wawili kati ya jamii ya Sara-Kaba, aliongeza Bw. Koulamallah. Wanaume 21 walikamatwa "na uchunguzi unaendelea kupata wahusika wote, wahusika wenza na washirika wa uhalifu huu", amehitimisha waziri.

Vurugu hizi hutokea mara kwa mara katikati na kusini mwa Chad, ambako wakazi wengi wana silaha. Wahamaji, wanaotoka katika maeneo kame ya Sahel ya kaskazini, pia wanazidi kutafuta kukaa kwenye ardhi inayofaa kwa ngamia na kondoo wao, kusinimwa nchi. Migogoro hii ya tangu mababu imeibuka tena katika miaka ya hivi karibuni katika eneo hili la bara, ikiathiri hasa Sudan, Sudan Kusini, Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Cameroon na Nigeria, sehemu za kusini au kaskazini ambazo zinapakana na ukanda wa Sahel.

Mnamo Machi 21, mamlaka ilionyesha kuwa angalau watu 42 waliuawa katika mapigano kati ya "jamii mbili" katika jangwa la mashariki mwa Chad, katika eneo ambalo wakulima wasio na shughuli na wafugaji wa kuhamahama hupigana mara kwa mara, au makundi mengine, kwa migogoro ya ardhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.