Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Mapigano mapya kati ya jamii mbili yazuka mashariki mwa Chad, watu 42 wauawa

Takriban watu 42 wameuawa katika mapigano kati ya "jamii mbili" katika jangwa mashariki mwa Chad, imetangaza Wizara ya Usalama wa Umma, katika eneo ambalo wakulima wasio na kazi na wafugaji wa kuhamahama, au makundi mengine, wanakabiliana kwa migogoro ya ardhi.

Raia wa Cameroon waliokimbia mapigano ya kikabila, walikusanyika katika kituo cha wakimbizi cha muda, huko Ndjamena, Chad, Alhamisi Desemba 9, 2021.
Raia wa Cameroon waliokimbia mapigano ya kikabila, walikusanyika katika kituo cha wakimbizi cha muda, huko Ndjamena, Chad, Alhamisi Desemba 9, 2021. © REUTERS - MAHAMAT RAMADANE
Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya, ambayo taarifa ya Wizara ya Usalama wa Umma haisemi ni kati ya makundi gani hasa au yalidumu kwa muda gani, pia yalisababisha "kukamatwa kwa watu 175 moja kwa moja kwenye eneo la uhalifu", ambapo "sehemu kubwa" ya kijiji cha Tileguey, katika jimbo la Ouaddaï, "limechomwa moto na watu wenye silaha".

"Hali imedhibitiwa lakini ninatafuta kupatanisha pande tofauti," amesema Waziri wa Usalama wa Umma, Jenerali Mahamat Charfadine Margui, katika ujumbe wa simu kwa shirika la habari la AFP, ambaye yuko kwenye eneo la tukio, akiongoza ujumbe wa serikali na wa jeshi ili "kutoa mwanga" juu ya tukio hili jipya.

Aina hizi za mapigano hatari sana hutokea mara kwa mara mashariki na kusini mwa nchi hii kubwa ya nusu jangwa huko Sahel. Mara nyingi huhusisha wafugaji wa kuhamahama wa Kiarabu dhidi ya wakulima wa kiasili wasiofanya kazi. Wafugaji wakipitisha au kuchunga mifugo yao katika mashamba ya watu wakulima, au jamii za wenyeji zinazobishana kuhusu kumiliki baadhi ya sehemu za ardhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.