Pata taarifa kuu
USAFIRI-HAKI

Nairobi: Mmoja wa wafanyakazi wawili wa Kenya Airways ameachiliwa DRC

Mmoja wa wafanyakazi wawili wa Shirika la Ndege la Kenya (KQ) waliokuwa wanazuiliwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu Aprili 19 ameachiliwa huru, afisa mkuu wa Kenya alisema Jumatatu.

Wafanyakazi hao wawili, waliokuwa wakifanya kazi katika ofisi ya shirika hilo la ndege mjini Kinshasa, walikamatwa Aprili 19 na idara ya ujasusi ya kijeshi, kulingana na Kenya Airways.
Wafanyakazi hao wawili, waliokuwa wakifanya kazi katika ofisi ya shirika hilo la ndege mjini Kinshasa, walikamatwa Aprili 19 na idara ya ujasusi ya kijeshi, kulingana na Kenya Airways. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ninashukuru sana kuwafahamisha kwamba Lydia Mbotela, mkuu wa KQ nchini DRC, ameachiliwa hivi punde na mamlaka mjini Kinshasa," Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje wa Kenya Korir Sing'oei alisema kwenye mtandao wa kijamii. Hakutoa habari kuhusu hatima ya mtu wa pili.

Wafanyakazi hao wawili, waliokuwa wakifanya kazi katika ofisi ya shirika hilo la ndege mjini Kinshasa, walikamatwa Aprili 19 na idara ya ujasusi ya kijeshi, kulingana na Kenya Airways.

Shirika la ndege la Kenya Airways lilikuwa limedai kuwa "sababu ya kukamatwa kwao ni kukosekana kwa hati za forodha zinazohusiana na shehena ya thamani ambayo ingesafirishwa kwa ndege ya KQ mnamo Aprili 12."

Lakini shehena hii "haikupakiwa wala kukubaliwa na KQ kutokana na kutokamilika kwa faili", lilibainisha shirika la ndege la Kenya Airways, likisikitika kwamba "jitihada zote za kuwaeleza maafisa wa kijeshi kwamba KQ haikukubali shehena hiyo kutokana na kutokamilika kwa nyaraka, zilikweda kombo".

Wafanyakazi hao walizuiliwa "bila mawasiliano hadi Aprili 23, wakati maafisa wa ubalozi na timu ya KQ waliruhusiwa kuwatembelea," kulingana na kampuni hiyo. Shirika la ndege la Kenya Airways lilitangaza mnamo Aprili 29 kwamba lilisitisha safari zake za ndege kuelekea Kinshasa, kutokana na kuzuiliwa "kinume cha sheria" kwa wafanyakazi wake wawili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mamlaka ya Kongo haijatoa taarifa yoyote kuhusu kukamatwa kwa watu hao . Kenya Airways ilianzishwa mwaka 1977 baada ya kufariki kwa shirika la ndege la Afrika Mashariki. Inafanya safari zake katika nchi 45, ikijumuisha 37 barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.