Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Côte d'Ivoire: Rais wa Senegal anataka 'kuondoa mtafaruku' katika ECOWAS

Rais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, anataka "kuondoa mtafaruku" ndani ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), wakati wa ziara yake siku ya Jumanne mjini Abidjan, ambako amekutana na mwenzake wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara.

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye na Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya rais mjini Abidjan Mei 7, 2024.
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye na Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya rais mjini Abidjan Mei 7, 2024. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwezi Januari, Burkina Faso, Niger na Mali, nchi tatu za Afrika Magharibi zikiongozwa na tawala za kijeshi zilizotokana na mapinduzi ya kijeshi, zilitangaza kujiondoa kwa ECOWAS, ambayo wanaituhumu kuwa chini ya ushawishi wa Ufaransa na kutowaunga mkono vya kutosha katika kupambana na wanajihadi. 

"Nina hakika kwamba ni lazima tuendelee kufanya kazi kwa mshikamano ndani ya eneo la ECOWAS, kufanya mageuzi yanayohitajika na kufanya kazi ili kuondoa sintofahamu ambayo haiwezi kushindwa kutokea," amesema Bassirou Diomaye Faye wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne. ECOWAS "ni chombo cha kipekee cha ushirikiano" ambacho "tutanufaika kutokana na kukihifadhi," ameongeza mkuu wa nchi, aliye madarakani tangu mwanzoni mwa mwezi Aprili.

Mali, Burkina Faso na Niger pia walijadili kufuta faranga ya CFA na kuunda sarafu ya pamoja kwa nchi zao tatu. Wakati wa kampeni zake za urais, Bassirou Diomaye Faye, mgombea mwenye umri wa miaka 44, pia alipendekeza kuachana na faranga ya CFA, sarafu inayotumiwa sasa na nchi nane za Afrika Magharibi (Senegal, Mali, Burkina, Niger, Côte d'Ivoire, Togo, Benin na Guinea-Bissau). "Katika ngazi ya kanda, changamoto ni nyingi, ni kubwa," rais wa Senegal amesema.

"Tuko katika hatua ya mabadiliko ambapo lazima tupime uzito wa vitisho vya kweli na kupungua kwa Mataifa, pamoja na hatari ya kusambaratika kwa muungano wetu," ameongeza. Nchi kadhaa za Afrika Magharibi, kama vile Burkina Faso, Mali na Niger, ndizo zinazolengwa na machafuko ya mara kwa mara ya wanajihadi ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya raia na wanajeshi.

Katika mpango wa nchi mbili, Bassirou Diomaye Faye na Alassane Ouattara wote wameelezea uhusiano kati ya nchi zao kama "bora". "Bado tunaweza kufanya zaidi, katika sekta ya kilimo", lakini pia katika ufugaji wa mifugo, ulinzi na usalama, amesema Bw. Faye.

Alassane Ouattara, pia anataka "kuimarisha" mahusiano haya, baada ya "kukaribisha kufanyika katika mazingira mazuri kwa uchaguzi wa urais nchini Senegal". Rais Faye alimrithi Macky Sall aliyeondoka baada ya ushindi katika duru ya kwanza dhidi ya mgombea wa serikali, Waziri Mkuu wa zamani Amadou Bâ.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.