Pata taarifa kuu

Senegal: Bassirou Diomaye Faye ameibuka mshindi kwa mujibu wa matokeo ya awali

Nairobi – Matekeo ya uchaguzi wa urais nchini Senegal ambayo yanasubiri kuthibitishwa na tume ya uchaguzi yanaonesha mgombea wa upinzani Bassirou Diomaye Faye ameibuka na ushindi wa asilimia 54.2 katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mpinzani,  tangu Senegal kujinyakulia uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960, kushinda uchaguzi katika duru ya kwanza
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mpinzani,  tangu Senegal kujinyakulia uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960, kushinda uchaguzi katika duru ya kwanza AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Tume ya uchaguzi  nchini Senegal imemtangaza Faye kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa asimilia 54, mahakama ya juu zaidi nchini Senegal sasa ikitarajiwa kuidhinisha matekeo hayo,  huku Amadou Ba, akijizolea asilimia 35.7 pekee ya kura zote zilizopingwa.

Faye amechaguliwa siku 10 tu baada ya kuachiliwa kutoka jela, na katika hutuba yake kwa raia wa Senegal amesema anahitaji kuweko kikomo kwa utawala wa sasa.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mpinzani,  tangu Senegal kujinyakulia uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960, kushinda uchaguzi katika duru ya kwanza.

Muda wa rais wa sasa kuhudumu unatarajiwa kukamilika Aprili 2, japo kwa mujibu wa katiba ya Senegal, wagombea wengine wa urais wakiwa na saa 72, kupingwa ushindi wa Faye, katika mahakama ya juu zaidi nchini humo baada ya matekeo hayo rasmi kutangazwa.

Mahakama hiyo itakuwa na siku tano kudhinisha au kufuta matekeo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.