Pata taarifa kuu
SIASA-MARIDHIANO

Wanasiasa wapongeza uamuzi wa rais wa kuwasamehe wafungwa

Wanasiasa nchini Côte d'Ivoire wamekaribisha siku ya Ijumaa uamuzi uliochukuliwa siku moja kabla na Rais Alassane Ouattara wa kuwasamehe wafungwa 51, wengi wao waliohusika katika machafuko ambayo nchi hiyo inapitia tangu 2010.

Gari la kikosi cha maafisa wa usalama linaingia kwenye gereza la Abidjan.
Gari la kikosi cha maafisa wa usalama linaingia kwenye gereza la Abidjan. SIA KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo (2000-2011) alionyesha "kuridhishwa kwake na kitendo hiki ambacho kinajumuisha hatua nzuri kuelekea upatanisho wa kitaifa uliosubiriwa kwa muda mrefu". Katika taarifa kwa vyombo vya habari, chama chake cha upinzani cha kisiasa, African People's Party Côte d'Ivoire (PPA-CI) "kinakaribisha uamuzi huu" huku kikitaja "hatu nzuri ambayo bado haijakamilika" kwa "wale ambao bado wanazuiliwa jela".

Miongoni mwa watu 51 waliosamehewa na Mkuu wa Nchi kwa "kutunza na kuimarisha amani" ni wahusika katika mgogoro wa baada ya uchaguzi wa 2010-2011 ambapo mapigano kati ya kambi ya Bw Gbagbo na ile ya Bw Ouattara yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000. Kuachiliwa kwao kulikuwa kumeombwa kwa miaka kadhaa na Laurent Gbagbo, mwenyewe aliyesamehewa mnamo mwezi wa Agosti 2022.

"Ningependa kupongeza hatua hii ya msamaha ambayo ilichukuliwa na Mkuu wa Nchi na kusema asante kwa hatua hii ya ujasiri iliyochukuliwa", ametangaza Charles Blé Goudé, wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Rais wa Pan-African Congress for Justice and Equality of Peoples (Cojep), hata hivyo, alisikitika kwamba raia "na ammbao sio muhimu hata kidogo" "wameachiliwa", akimaanisha hasa kesi yake binafsi. "Wakati wangu utafika," ameongeza.

Akiwa ameachiliwa na haki ya kimataifa kwa jukumu lake wakati wa mzozo wa 2010-2011, kama vile mshauri wake wa zamani Laurent Gbagbo, Charles Blé Goudé bado amehukumiwa nchini mwake miaka 20 jela, hukumu ambayo haijatekelezwa tangu kurudi kwake mwaka 2022. Hayumo kwenye orodha ya watu 51 waliosamehewa.

Kwa upande mwingine, tunaona Brunot Dogbo Blé, alihukumiwa mwezi Aprili 2017 hadi miaka 18 jela kwa kuhusika kwake katika suala la "watu waliotowekakatika hoteli ya Novotel", mauaji ya watu wanne ikiwa ni pamoja na watu wawili, raia Ufaransa mwezi Aprili 2011.

Washirika wa karibu wa Waziri Mkuu wa zamani Guillaume Soro, mshirika wa zamani wa Alassane Ouattara ambaye sasa ana utata na rais Ouattara na ambaye yuko uhamishoni, pia wanahusikana uamuzi huo wa msamaha wa rais. Lakini kwa baadhi ya watetezi wa haki za waathiriwa wa mgogoro huu, hatua hizi ni za kukatisha tamaa.

"Hii inahitimisha uwezekano wote tuliokuwa nao kupata fidia ya kisheria kwa waathiriwa" wa mgogoro huo, anasikitika Willy Neth, mkuu wa shirika la Haki za Kibinadamu  nchini Côte d' Ivoire (Lidho). "Ni haki pekee inayoweza kuleta upatanisho wa kudumu," anaongeza kwa shirika la habari la AFP. Mnamo mwaka wa 2018, serikali ya Côte d'Ivoire ilipitisha sheria kubwa ya msamaha kwa jina la upatanisho wa kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.