Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Côte d'ivoire: Matokeo ya uchaguzi yasubiriwa, siku moja baada ya uchaguzi

Karibu wapiga kura milioni 8 waliitwa kupiga kura jana (Jumamosi) kuchagua mameya na viongozi wa mabaraza ya kikanda nchini Côte d'Ivoire. Huu ni uchaguzi wa mwisho kabla ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2025. Uchaguzi huu unafuatiliwa kwa karibu. Ulifanyika kwa amani. Hata hivyo, matukio kadhaa yaliripotiwa usikuwa kuamkia Jumapili.

Uchaguzi wa serikali za mitaa ulifanyika kwa tulivu, Jumamosi Septemba 2, nchini Côte d'Ivoire. Kura iliyofuatwa kwa karibu kwa sababu inachukuliwa kuwa puto ya majaribio kwa uchaguzi wa urais wa 2025. Matokeo yatajulikana kufikia Jumatatu.
Uchaguzi wa serikali za mitaa ulifanyika kwa tulivu, Jumamosi Septemba 2, nchini Côte d'Ivoire. Kura iliyofuatwa kwa karibu kwa sababu inachukuliwa kuwa puto ya majaribio kwa uchaguzi wa urais wa 2025. Matokeo yatajulikana kufikia Jumatatu. REUTERS - LUC GNAGO
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumamosi, kulikofanyika uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Côte d'Ivoire kwa ujumla ilielezwa kuwa uchaguzi ulifanyika kxa utulivu na amani. Jumamosi jioni, mkuu wa jeshi alisema kwamba hakuna tukio kubwa lililoripotiwa lakini, usiku, hitilafu kadhaa zilibainishwa na waangalizi. Kulingana na Baraza la Kitaifa la Haki za Kibinadamu, katika eneo la Moronou kwa mfano, huko M'batto, mkuu wa kituo cha kupigia kura alisitisha zoezi la kuhesabu kura na alirejea nyumbani karibu kumi na dakika 56 Alfajiri. Huko Mankono, masanduku manne ya kura yaliporwa na huko Marahoué, kulikuwa na uharibifu wa mali ya umma. Ofisi ya  Tume Huru ya Uchaguzi (CEI) katika eneo hilo iliripotiwa kuwekwa chini ya ulinzi wa jeshi. Hizi hapa taarifa za hivi punde za asubuhi ya Jumapili hii, Septemba 3.

Baadhi ya askari na maafisa wa polisi 4,400 walitumwa kulinda vituo vya kupigia kura. Pia wamekuwepo wakati wa kukusanya na kusafirisha vifaa vya uchaguzi, anabainisha mwandishi wetu wa Abidjan, Bineta Diagne.

Baraza la Kitaifa la Haki za Kibinadamu limebaini takriban visa 250 vya matukio yanayohusishwa na kuchelewa kuwasili kwa vifaa vya uchaguzi na kuchelewa kufunguliwa kwa baadhi ya vituo vya kupigia kura. Kando na mizozo ya ndani katika wilaya za Plateau na Marcory, hakuna kitendo kikubwa cha vurugu kilichoripotiwa Jumamosi alasiri.

Huko Yopougon, wilaya yenye wakazi wengi zaidi katika mkoa wa Abidjan, inayochukuliwa kuwa wilaya yenye maamuzi kwa vyama vya kisiasa, kura ilifanyika kwa utulivu. RFI ilikutana na wapiga kura kutoka mji huu, kama Anastasie ambaye alipiga kura kwa mara ya pili maishani mwake.

Muungano wa Mashirika ya Kiraia ulielezea mazingira ya "amani". shirika la kiraia la Cosel-CI imerekodi takriban matukio mia moja, ambayo hayakuzuia mchakato wa uchaguzi.

Siku tulivu ya kupiga kura huko Adzopé

Usiku kucha, matokeo katika mikoa 31 na manispaa 201 yalikusanywa na Tume Huru ya Uchaguzi. Huko Adzopé, kusini-mashariki mwa nchi, karibu kilomita mia moja kutoka Abidjan, uchaguzi ulifanyika kwa amani, anaripoti mwandishi wetu maalum, François Hume-Ferkatadji.

Mitindo ya ushiriki bado haijawekwa wazi. Lakini jana, rais aliwahimiza raia wa côte d'Ivoire kuhamasishwa: kiwango cha ushiriki katika chaguzi zilizopita za mitaa si cha juu sana, kinabadilika kati ya 35 na 40%, amebainisha rais Alassane Ouattara.

Matokeo ya chaguzi hizi za mitaa yanatarajiwa kutangazwa siku ya Jumapili hii, Septemba 3.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.