Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-UTEUZI

Côte d’Ivoire: Robert Beugré Mambé ateuliwa kuwa Waziri Mkuu

Robert Beugré Mambé ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Côte d'Ivoire Jumatatu hii, Oktoba 16, 2023, ofisi ya rais wa Côte d’Ivoire imetangaza. Robert Beugré Mambé alikuwa mkuu wa wilaya inayojitawala ya Abidjan. Robert Beugré Mambé ni nambari tatu kwa sasa katika katika chama tawala cha RHDP.

Waziri Mkuu mpya wa Côte d'Ivoire Robert Beugré Mambé (kulia) akiwa na rais wa nchi hiyo, Alassane Ouattara.
Waziri Mkuu mpya wa Côte d'Ivoire Robert Beugré Mambé (kulia) akiwa na rais wa nchi hiyo, Alassane Ouattara. © Présidence de Côte d'Ivoire
Matangazo ya kibiashara

Siku kumi na moja baada ya mabadiliko ya serikali, ofisi ya rais ndiyo imetoa jina la Waziri Mkuu mpya, Oktoba 16, 2023. Kiongozi huyo mpya wa serikali ni Robert Beugré Mambé. Ni afis wa ngazi ya juu katika chama tawala cha RHDP. Hivi majuzi alichaguliwa kuwa meya wa Songon wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mnamo Septemba 2.

Robert Beugré Mambé alikuwa mkuu wa wilayaya Abidjan tangu 2011: kazi yake, hapo awali, katikati ya mzozo wa baada ya uchaguzi, ilikuwa kurudisha mshikamano wa kijamii na kujenga upya "Abidjan", kupitia miundombinu ya miradi, hasa. Ni mwanasiasa mchapa kazi, anayejulikana sana katika mji mkuu wa kiuchumi. Hapo awali, alikuwa mkurugenzi katika ofisi za mawaziri kadhaa. Pia aliongoza Tume Huru ya Uchaguzi…

Robert Beugré Mambé amekuwa akiombwa mara kadhaa na Benki ya Dunia kuongoza miradi ya maendeleo. Robert Beugré Mambé pia ni sehemu ya Jumuiya ya Kimataifa ya Mameya wanaozungumza Kifaransa…

Uteuzi wa kushtukiza

Uteuzi wake umewashangaza wengi. Katika siku za hivi karibuni, uvumi umetoa majina kadhaa. Lakini hadi dakika ya mwisho, hakuna kitu, chochote kabisa, kilikuwa kimevuja kuhusu chaguo hili. "Hakuna aliyetarajia uteuzi huu," waziri ameiambia RFI.

Robert Beugré Mambé sasa ana jukumu la kufafanua timu mpya ya serikali. Na kwa kiwango hiki, mchezo unabaki kuwa wazi, kwani katika Baraza la Mawaziri, wiki tatu zilizopita, Alassane Ouattara alibaini kwamba  ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa Septemba 2 haukuwa kigezo chake: rais anaunda tena timu yake kuandaa chama cha RHDP kwa uchaguzi ujao wa urais mnamo mwaka 2025.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.