Pata taarifa kuu
SHERIA-USALAMA

'Jaribio la mapinduzi' Sierra Leone: Watu kumi na wawili wafunguliwa mashtaka

Ofisi kuu ya mashitaka imemfungulia mashitaka Amadu Koita na watu wengine 11, wakiwemo maafisa wa zamani wa polisi, kwa "uhaini, kushiriki katika uhaini, kuhifadhi, kusaidia adui na kuchochea vurugu" wakati wa "jaribio la mapinduzi" la Novemba 26, imesema taarifailiyotiwa saini na Waziri wa Habari Chernor A. Bah.

Mapema Novemba 26, watu kadhaa walishambulia ghala la kijeshi, kambi nyingine mbili, magereza mawili na vituo viwili vya polisi, nchini Sierra Leone.
Mapema Novemba 26, watu kadhaa walishambulia ghala la kijeshi, kambi nyingine mbili, magereza mawili na vituo viwili vya polisi, nchini Sierra Leone. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Washukiwa kumi na moja tayari walifikishwa mbele ya jaji. Kesi ya mshukiwa wa kumi na mbili imeahirishwa hadi Januari 9 kwa sababu ya ugonjwa, inaongeza taarifa hii, ambapo washtakiwa wote wanasaidiwa na wakili.

Mapema Novemba 26, watu kadhaa walishambulia ghala la kijeshi, kambi nyingine mbili, magereza mawili na vituo viwili vya polisi, wakikabiliana na vikosi vya usalama wakitumia bunduki. Mapigano hayo yalisababisha vifo vya watu 21, askari 14, askari polisi mmoja, askari magereza, afisa wa usalama, mwanamke mmoja na washambuliaji watatu, kwa mujibu wa Waziri wa Habari.

Kanda ya Afrika Magharibi inakabiliwa tangu 2020 na ongezeko la mapinduzi ya kijeshi. Nchi za Mali, Burkina Faso, Niger na Guinea, zilikumbwa na majaribio kadhaa ya mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.