Pata taarifa kuu

Jaribio la mapinduzi: Rais wa zamani wa Sierra Leone aitishwa na polisi

Rais wa zamani wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ametishwa na polisi siku ya Alhamisi ndani ya saa 24 kuhojiwa kuhusu matukio ya Novemba 26, yaliyoelezwa kama jaribio la mapinduzi ya serikali, shirikala habari la AFP limenukuu chanzo kutoka Wizara ya Habari ya Sierra Leone.

Ernest Bai Koroma, rais wa zamani wa Sierra-Leone.
Ernest Bai Koroma, rais wa zamani wa Sierra-Leone. (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Bw Koroma, ambaye aliongoza Sierra Leone kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2018, anatazamiwa kuzuru makao makuu ya Idara ya Upelelezi wa Jinai huko Freetown, mji mkuu. "Ameitwa kusaidia polisi katika uchunguzi unaoendelea" katika matukio ya Novemba 26, inasema taarifa iliyotiwa saini na Waziri wa Habari, Chernor A. Bah. Mkuu huyo wa zamani wa huduma za serikali amethibitisha kuitwa kwake katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa kutoka Makeni, mji wa kaskazini mwa Sierra Leone ambako alikuwa siku ya Alhamisi kulingana na wasaidizi wake.

Mtangulizi wa rais wa sasa, Julius Maada Bio, anasema katika taarifa hii kwamba atakwenda Freetown, bila kutaja tarehe. "Nina mawazo wazi na niko tayari kushirikiana kikamilifu na polisi katika uchunguzi wao. Utawala wa sheria lazima utawale katika demokrasia yetu," amesema, akinukuliwa katika taarifa hii. Anatoa wito wa utulivu na kuwataka watu kuunga mkono uchunguzi wa polisi.

Walinzi wa zamani wa Bw. Koroma, kulingana na mamlaka ya Sierra Leone, wanashukiwa kushiriki katika machafuko ya Novemba 26. Mapema siku hiyo, watu walishambulia ghala la kijeshi, kambi mbili, magereza mawili na vituo viwili vya polisi.

Mapigano hayo yalisababisha vifo vya watu 21, maafisa 18 wa idara ya usalama na washambuliaji watatu, kulingana na Waziri wa Habari. Watu sitini walikamatwa kuhusiana na matukio haya, hasa askari, kulingana na takwimu zilizotolewa na mamlaka.

Kanda ya Afrika Magharibi imekuwa na inakumbwa mapinduzi ya kijeshi tangu mwaka 2020, nchini Mali, Burkina Faso, Niger na Guinea. Jumamosi jioni, Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo pia alishutumu "jaribio la mapinduzi" katika nchi yake baada ya mapigano kati ya jeshi na maafisa wa usalama usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.