Pata taarifa kuu

Mkutano wa kilele wa Johannesburg: BRICS wakubaliana juu ya kanuni ya upanuzi

Mkutano wa 15 wa BRICS umeendelea siku ya Jumatano, Agosti 23 katika eneo la Sandton huko Johannesburg. Katika siku hii ya pili, viongozi wa nchi tano wanachama wa muungano huo wameingia katika undani wa mada, wakijadili mustakabali na matarajio ya kuendelezwa kwa makubaliano yao.

Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza kwa njia ya video wakati wa mkutano wa kilele wa BRICS 2023 kwenye Kituo cha Mikutano cha Sandton huko Johannesburg mnamo Agosti 23, 2023. Nyuma ni rais wa China Xi Jinping.
Rais wa Urusi Vladimir Putin akizungumza kwa njia ya video wakati wa mkutano wa kilele wa BRICS 2023 kwenye Kituo cha Mikutano cha Sandton huko Johannesburg mnamo Agosti 23, 2023. Nyuma ni rais wa China Xi Jinping. AFP - GIANLUIGI GUERCIA
Matangazo ya kibiashara

Nchi tano wanachama wa BRICS, ambazo ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, wanaokutana katika mkutano wa kilele mjini Johannesburg, wamekubaliana Jumatano hii, katika siku ya pili ya mkutano wa kilele wa muungano huu wa nchi zinazoinukia, upanuzi wa muungano huu wa BRICS. Lakini uchaguzi wa kimkakati wa wanachama wapya bado itabidi kujadiliwa.

“Tumekubaliana kuhusu suala la upanuzi. Tumepitisha waraka ambao unaweka miongozo, kanuni na taratibu za mapitio kwa nchi zinazotaka kuwa wanachama wa BRICS,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor ameiambia redio ya taifa matokeo ya majadiliano.

Mazungumzo mengi yalifanyika katika kikao kilichofungwa kwa vyombo vya habari, amesema mwandishi wetu maalum katika mkutano huo, Claire Bargelès. Viongozi hao walizungumza hapo awali asubuhi, yote kwa ujumla yakiwa tayari kupanua kundi hilo, wakati dunia inatikisika na "zama mpya ya misukosuko na mabadiliko", kulingana na Xi Jinping.

.Viongozi watano - Vladimir Putin hayupo Afrika Kusini - wanapaswa kuzungumza, Alhamisi mchana, na nchi za Kusini zinazojulikana kama "marafiki". Takriban viongozi thelathini wa Afrika wakiwemo wakuu wa nchi za Senegal, Ethiopia na Ghana watakuwepo kwa siku ya mwisho ya mkutano huu wa 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.