Pata taarifa kuu

Maandamano mjini Tunis kupinga kuhojiwa kwa waandishi wa habari na polisi

Makumi ya waandishi wa habari walikusanyika mjini Tunis siku ya Jumatatu kupinga polisi kuwasikiliza na kuwahoji waandishi wawili wa habari kutoka kituo cha redio cha kibinafsi kwa kutaja katika makala yao mapungufu katika kuajiriwa maafisa wapya ndani ya idara za usalama.

Waandishi wa habari wa Tunisia walikusanyika mjini Tunis kwa ajili ya maandamano ya uhuru wa vyombo vya habari mnamo Februari 16, 2023, siku nne baada ya kukamatwa kwa Noureddine Boutar, mkurugenzi mkuu wa Mosaïque FM.
Waandishi wa habari wa Tunisia walikusanyika mjini Tunis kwa ajili ya maandamano ya uhuru wa vyombo vya habari mnamo Februari 16, 2023, siku nne baada ya kukamatwa kwa Noureddine Boutar, mkurugenzi mkuu wa Mosaïque FM. AP - Hassene Dridi
Matangazo ya kibiashara

Walikusanyika mbele ya makao makuu ya kikosi cha polisi kinachosimamia kesi za uhalifu ili kuwaunga mkono wenzao Haythem El Mekki na Elyes Gharbi kutoka Mosaïque FM waliosikilizwa, kulingana na waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Wanahabari hao wawili waliitwa kufuatia malalamiko yaliyotolewa na chama cha polisi kwa kutaja katika kipindi chao maarufu cha Midi-Show, Mei 15, mapungufu katika kuajiriwa maafisa wapya ndani ya idara za usalama, baada ya afisa wa polisi kuua kwa kuwapiga risasi watu watano, wakiwemo mahujaji wawili wa Kiyahudi nje ya sinagogi kwenye kisiwa cha Djerba mnamo Mei 9. Muungano unaohusika na malalamiko hayo unawashutumu wanahabari hao kwa kuhatarisha usalama vikosi vya usalama.

"Vitimbi na vitisho dhidi ya wanahabari vinaendelea nchini Tunisia na sera hii kandamizi ambayo inataka kunyamazisha kila mtu," Amira Mohamed, naibu kiongozi wa Chama cha Wanahabari (SNJT), ameliiambia shirika la habari la AFP. Kulingana na SNJT, karibu waandishi wa habari ishirini wanashitakiwa kwa kazi yao.

Mkurugenzi wa Mosaïque FM, Noureddine Boutar, amezuiliwa tangu mwezi Februari pamoja na watu wengine wanaotuhumiwa "kula njama dhidi ya usalama wa taifa". Mwandishi mwingine wa Mosaïque FM alihukumiwa kwa rufaa katikati ya mwezi Mei hadi miaka mitano jela chini ya sheria ya kupambana na ugaidi kwa kufichua habari kuhusu operesheni iliyofanywa na idara za usalama.

Wanahabari kadhaa waliandamana Alhamisi kupinga hukumu hii na kulaani wanasiasa kushawishi vyombo vya sheria na kutishia vyombo vya habari. Mashirika kadhaa ya ndani na kimataifa yanashutumu kupungua kwa uhuru nchini Tunisia tangu Rais Kais Saied achukue mamlaka kamili mnamo Julai 25, 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.