Pata taarifa kuu
TUNISIA-USALAMA

Tunisia: Waandishi wa habari kadhaa washambuliwa na polisi

Nchini Tunisia, waandishi wa habari kadhaa walinyanyaswa na polisi siku ya Ijumaa tarehe 14 Januari. Miongoni mwao, mwandishi wa RFI Mathieu Galtier. Alikuwa akiripoti, kwa niaba ya gazeti la Ufaransa la Liberation, maandamano dhidi ya Rais Kaïs Saïed.

Vikosi vya usalama vilitawanya maandamano yaliyoandaliwa dhidi ya rais Ijumaa, Januari 14, 2022 huko Tunis licha ya marufuku ya mikusanyiko kwa sababu za kiafya.
Vikosi vya usalama vilitawanya maandamano yaliyoandaliwa dhidi ya rais Ijumaa, Januari 14, 2022 huko Tunis licha ya marufuku ya mikusanyiko kwa sababu za kiafya. AFP - FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo, yaliyoitishwa na upinzani na kupigwa marufuku na serikali kwa sababu ya ugonjwa hatari wa Covid, pia yalilenga kuadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi ya kuanguka kwa utawala wa rais wa zamani Ben Ali.

Mwenzetu Mathieu Galtier, ambaye pia ni ripota wa vyombo kadhaa vya habari vya Ufaransa, aliangushwa chini na maafisa kadhaa wa polisi. Walimpokonya simu yake na kadi yake ya kazi, ambayo alirudishiwa baadaye.

Kwa upande mwingine, kadi ya kumbukumbu ya simu yake ambayo picha za video za maandamano na ukandamizaji wa polisi zilirekodiwa haikupatikana. Mathieu Galtier alipewa siku 15 za kupumzika na daktari ambaye alibainisha jeraha kwenye paji la uso.

“Tunalaani vikali uvamizi huu wa polisi dhidi ya mwanahabari hapa Tunis. Tumeomba kufunguliwa kwa uchunguzi katika Wizara ya Mambo ya Ndani. Vitendo hivi sio vya kufumbia macho, amesema Alaa Talbi, mmoja wa viongozi wa shirika la Haki za Kiuchumi na Kijamii, akihojiwa na RFI.

Huyu sio mwanahabari wa kwanza kushambuliwa, na kilichotokea jana kinathibitisha kwa mara nyingine kwamba mfumo wa polisi au serikali ya polisi bado inatawala nchini Tunisia, hata miaka kumi baada ya mapinduzi. Bado tupo kwenye mazoea yale yale, bado tuko kwenye kutoheshimu haki za binadamu, katika kutoheshimu haki ya maandamano na pia tuko kwenye ukweli hasa kwamba hatupo katika kuwasaidia waandishi wa habari kufichua ukweli na kufanya kazi yao. 

Uongozi wa RFI unaungana na gazeti la kila siku la Libération kulaani vikali shambulio hili la polisi dhidi ya mwanahabari wetu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.