Pata taarifa kuu

Sudan: Raia wakabiliwa na changamoto za kiuchumi mapigano yakiripotiwa Khartoum

NAIROBI – Nchini Sudan, mapigano yameendelea leo jijini Khartoum kati ya wanajeshi na wanamgambo wa RSF, huku raia wa kawaida wakiendelea kuhangaika kwa kukosa mahitaji muhimu ya kibinadamu.

Raia wa Sudan wanazidi kukabiliwa na ugumu wa maisha wakati huu mapigano yakiripotiwa kuendelea
Raia wa Sudan wanazidi kukabiliwa na ugumu wa maisha wakati huu mapigano yakiripotiwa kuendelea © Marwan Ali / AP
Matangazo ya kibiashara

Wakaazi wa Khartoum, kwa siku kadhaa sasa wameendelea kuishi bila umeme na mahitaji mengine muhimu kama chakula na maji, huku watoa misaada nao wakishindwa kuwasaidia raia wa kawaida, kwa sababu ya vuta vinavyoendelea.

Nalo Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema chakula chenye thamani ya kati ya Dola 13 hadi 14 kilichokuwa kiwasaidie watu, kimebiwa.

Maelewano ya kusitisha vita kwa siku saba, yanaonekana kutoheshimiwa kati ya pande hizo mbili, huku mapambano yakiendelea kudhibiti makao makuu ya jeshi na Ikulu ya rais.

Mapigano yanaendelea wakati huu rais wa Marekani Joe Biden, akitoa idhini ya watu wanaochochea mapigano hayo kuwekewa vikwazo, akisema ni sharti vita vinavyoendelea vikome.

Shirika la umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi, UNHCR limesema kwamba takriban dola milioni 445 zinahitajika ili kuwasaidia watu ambao wanakadiriwa huenda wakakimbia Sudan kufikia mwezi Oktoba, kutokana na mapigano yanayoendelea.

UNHCR sasa inatoa wito kwa nchi wafadhili kusaidia katika upatikanaji wa fedha hizo.

Umoja wa Mataifa unasema hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya, na inataka pande zinazopigana, kutoa hakikisho la usalama wa wafanyakazi na misafara iliyobeba misaada ya kibinadamu kama chakula na dawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.