Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Kiongozi wa Boko Haram ajeruhiwa baada ya kujaribu kujiua

Kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, Abubakar Shekau amejeruhiwa wakati alipokuwa anajaribu kujiua kuepuka kukamatwa, wakati wa makabiliano makali na kundi pinzani la kijihadi, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Abubakar Shekau, kiongozi wa Boko Haram.
Abubakar Shekau, kiongozi wa Boko Haram. Handout BOKO HARAM/AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Ripoti za Kiinteljesia zinasema kuwa, kundi la Boko Haram chini ya Shekau limekuwa katika makabiliano na kundi la Islamic State, ISWAP, linaloendeleza harakati zake Afrika Magharibi, katika jimbo la Borno.

Inaelezwa kuwa mapigano hayo yalitokea katika msitu wa Sambisa, kwenye ngome kuu ya Boko Haram, huku wapiganaji wake wakikimbilia kusikojulikana.

Aidha, ripoti nyingine ya kiiteljensia inaeleza kuwa Shekau alijeruhiwa baada ya kushambuliana na wapiganaji wake katika nyumba aliyokuwa amejificha na wapiganaji wake.

Shekau ambaye aligongwa vichwa vya Habari mwaka 2014 baada ya kuwateka wasichana karibu 300 wa shule ya wasichana ya Chibok, na amekuwa akiripotiwa mara kadhaa kuwa ameuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.