Pata taarifa kuu
UTURUKI-LIBYA-ITALIE-USALAMA

Ankara yakaribisha 'msimamo' wa Roma kwa Libya

Uturuki imetangaza leo Ijumaa kuwa itaendelea kushirikiana na Italia kufikia amani ya kudumu na mchakato wa kisiasa nchini Libya, na hivyo kukaribisha Roma kwa msimamo wake wa "kutojihusisha" na maswala ya Libya "tofauti na nchi zingine za Ulaya".

Vita nchini Libya imesababisha uharibifu mkubwa.
Vita nchini Libya imesababisha uharibifu mkubwa. Mahmud TURKIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Pamoja na Italia, tutaendelea na juhudi zetu kwa ajili ya amani ya kudumu na mchakato wa kisiasa wenye mafanikio nchini Libya," Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Ankara pamoja na mwenzake wa Italia, Luigi Di Maio.

"Tunafahamu jukumu muhimu la Italia katika suala hili na tunaishukuru kwa hilo. Italia imeonyesha msimamo mzuri wa kutopendelea upande wowote kati ya pande mbili hasimu zinazokinzana nchini Libya. Italia haikuiunga mkono Haftar, tofauti na nchi zingine za Umoja wa Ulaya, bali Italia ilifanya juhudi za dhati ili kufikia mkataba wa kusitisha mapigano na mchakato wa kisiasa, " Mevlut Cavusoglu ameongeza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki hakutaja nchi yoyote ya Umoja wa Ulaya ambayo inajihusisha katika masuala ya Libya na hususan inayounga mkono kambi ya Marshal Khalifa Haftar, lakini kauli yake inakuja baada ya mvutano wa kidiplomasia kati ya Uturuki na Ufaransa, ambayo inaishtumiwa kumuunga mkono Marshal Haftar. madai ambayo Paris inakanusha

Uturuki inaendelea kusaidia kijeshi majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, dhidi ya mashamblizi ya Marshal Khalifa Haftar ambaye anasaidiwa na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.