Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Libya: Mvutano waibuka kati ya Urusi na Uturuki

Urusi na Uturuki - ambazo zina jukumu kubwa la kusitisha mapigano nchini Libya - zinaonekana kuwa hazikubaliani kwa masharti ya mpango wa kudumu wa kusitisha mapigano.

Vikosi vya Khalifa Haftra mwaka 2019. Ankara inataka vikosi vinavyoongozwa na Khalifa Haftar kuondoka Benghazi.
Vikosi vya Khalifa Haftra mwaka 2019. Ankara inataka vikosi vinavyoongozwa na Khalifa Haftar kuondoka Benghazi. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili Juni 14, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, na mwenzake wa Ulinzi wa Uturuki, Sergei Shoigu, walikuwa wanasubiri mjini Istanbul; lakini ziara hii ilifutwa kwa dakika ya mwisho. Hakuna sababu iliyotolewa, lakini kulingana na vyombo vya habari vya Uturuki kauli za kutokubaliana zimeripotiwa kati ya nchi hizo mbili zinazounga mkono kambi zinazopingana nchini Libya.

"Mizozo yetu haihusu kanuni za msingi," imesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki baada ya kufutwa kwa ziara ya mawaziri wawili wa Urusi jijini Ankara: Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu.

Urusi na Uturuki zinaunga mkono kambi mbili zinazokinzana nchini Libya na Ankara inabaini kwamba imepiga hatua zaidi kwenye uwanja wa vita kuliko Moscow, ambayo imeamua kutoa masharti kwenye makubaliano ya kugawana madaraka na kuwezesha kusitisha mapigano nchini Libya.

Ankara imekataa pendekezo la Urusi na inaomba hali nchini Libya irudi kama ilivyo kuwa katika miaka ya 2015. Hiyo ni kusema, kuviondoa vikosi vya Khalifa Haftar kwenda Benghazi, jambo ambalo Moscow imefutilia mbali kabisa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.