Pata taarifa kuu
LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Urusi na Uturuki zashutumiwa kuchochea vita Libya

Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNA) imekataa katu katu kukaa kwenye meza ya mazungumzo na kambi ya Jenerali Khalifa Haftar, mbabe wa kivita Mashariki mwa nchi hiyo, kabla ya haijadhibiti miji miwili ya kimkakati ya Sirte na Al-Joufra.

Wapiganaji tiifu kwa Serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kuuweka tena kwenye himaya yao mji wa Tripoli, Juni 4, 2020.
Wapiganaji tiifu kwa Serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kuuweka tena kwenye himaya yao mji wa Tripoli, Juni 4, 2020. REUTERS/Ayman Al-Sahili
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Tripoli pia imekataa juhudi za Misri za kusitisha mapigano. Lakini shinikizo la kimataifa, hasa kutoka Urusi, linaiweka serikali hiyo tumbo joto na kukubali kuchangia madaraka, mkataba uliofikiwa hivi karibuni kati ya Moscow na Ankara.

Shinikizo kutoa Urusi na Uturuki zinaonekana hata kwenye uwanja wa kivita. Uturuki ikiungwa mkono na Marekani inasaidia serikali ya Tripoli inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, huku urusi ikiungwa mkono na baadhi ya nchi za kiarabu, ikisaidia vikosi vya Jenerali Khalifa Haftar.

Kambi ya kimkakati ya al-Witya na uwanja wa ndege wa Maitigua huko Tripoli, unaweza kuwa kambi ya jeshi la Kituruki na Marekani, Al-Joufra na Sirte kuwa ngome kuu za vikosi vya Urusi.

Hivi karibuni rais wa Misri Abel-Fattah al-Sissi alitangaza juhudi za kumaliza mzozo katika nchi jirani ya Libya.

Jeshi la Haftar linalojulikana kama Libyan Arab Armed Forces lililoko upande wa mashariki lilianzisha mashambulizi mwaka ulipita kuukamata mji mkuu Tripoli. Lakini hivi karibuni amepoteza maeneo muhimu ya kimkakati magharibi mwa Libya baada ya Uturuki kuongeza msaada wake kwa makundi kadhaa ya wanamgambo ambayo yanamafungamano na serikali yenye makao yake makuu mjini Tripoli.

Libya imekuwa katika machafuko tangu mwaka 2011 wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe viliposababishwa kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa muda mrefu Moammar Gaddafi, ambaye baadaye aliuwawa.

Nchi hiyo imegawanyika katika serikali hasimu upande wa mashariki na magharibi, kila moja ikiungwa mkono na makundi yenye silaha pamoja na serikali za kigeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.