Pata taarifa kuu
DRC-WHO-EBOLA-AFYA

DRC: Baada ya kesi ya Ebola Goma, WHO yaitisha kamati yake ya dharura

Virusi vya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), bado ni vigumu kudhibiti. Kwa mujibu wa Mkuu wa shirika la Afya Duniani (WHO), mtu mmoja kupatikana na virusi vya Ebola katika mji wa Goma, hali hiyo inaweza "kubadili maisha ya wakaazi wa mji huo."

Wajumbe wakishiriki mkutano wa WHO kuhusu Ebola DRC, Julai 15, 2019 Geneva.
Wajumbe wakishiriki mkutano wa WHO kuhusu Ebola DRC, Julai 15, 2019 Geneva. © FABRICE COFFRINI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Goma ni mji wenye watu milioni moja, pamoja na muingiliano wa watu kutoka miji mingine ya nchi hiyo na nchi jirani ya Rwanda. Kamati ya dharura ya shirika la Afya Duniani (WHO) inatarajiwa kukutana tena katika siku zijazo kuamua kama Ebola imekuwa tishio la kimataifa.

Kuuawa kwa watu wawili miongoni mwa maafisa wanaopambana dhidi ya ugonjwa wa Ebola katika mkowa wa Kivu Kaskazini na kupatikana kwa mtu mwenye virusi vya Ebola katika mji wa Goma, kumezua sintofahamu kwenye ajenda ya mkutano wa shirika la Afya Duniani uliofanyika Jumatatu, Julai 15, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Ikiwa ugonjwa huo umefika Goma, unaweza pia kufika katika mji mkuu Kinshasa.

Waziri wa Afya wa DRC, Oly Ilunga amewahakikishia wananchi wake. Amebaini kwamba hakuna hatari ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kwa kiwango kikubwa tangu kuonekana kwa virusi vya ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa wizara ya afya ya DRC, mtu huyo ambaye ni Mchungaji alisafiri umbali wa kilomita zaidi ya 200 kutoka Butembo hadi Goma kwa basi, na inasadikiwa kuwa alikuwa amekutana na watu wenye ugonjwa Ebola.

Ebola huwaathiri binaadamu kupitia mgusano na wanyama walioathirika kama tumbili, na popo wa msituni.

Watu huambukizwa kwa njia ya kugusana, njia ya mdomo na pua, pia kwa njia ya damu, matapishi, kinyesi, majimaji ya kwenye mwili wa mtu mwenye Ebola.

Ebola ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambapo aliyepata maambukizi hupata dalili za homa, uchovu, maumivu ya viungo na koo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.