Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Ebola yaua watu 1,500 DRC

Zaidi ya watu elfu 1 na 500 wameripotiwa kufa katika kipindi cha miezi 10 tangu kuripotiwa kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, wizara ya afya nchini humo imethibitisha.

Wafanyakazi wa kituo cha matibabu ya Ebola huko Butembo wakimuhudumia mwanamke aliye ambukizwa virusi vya Ebola, Machi 28, 2019.
Wafanyakazi wa kituo cha matibabu ya Ebola huko Butembo wakimuhudumia mwanamke aliye ambukizwa virusi vya Ebola, Machi 28, 2019. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine vijana waliokuwa na hasira wameripotiwa kuchoma moto vituo vitatu vilivyokuwa vinatoa matibabu ya Ebola pamoja na kuharibu magari ya wagonjwa jijini Beni.

Mlipuko wa Ebola DRC mashariki ni wa pili kwa ukubwa katika historia.

Shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto, UNICEF, linasema mlipuko huu ni wa 10 kutokea nchini DRC na ni mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo na ni wa pili kwa ukubwa kuwahi kushuhudiwa kwenye historia ukiongozwa na mlipuko wa ebola huko Afrka Magharibi kati ya mwaka 2014-2016.

Kumekuwa na ongezeko la visa vya Ebola katika jimbo la kivu kaskazini nchini DRC, hususan kwenye eneo la Katwa ambapo timu za kukabiliana na mlipuko zimekumbwa na ukosefu wa imani kutoka kwa wanajamii, mlipuko umekwenda hadi maeneo ya Kayina ambako hali ya usalama ni hatarishi, kwa mujibu wa Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Chini ya kampeni iliyozinduliwa tarehe 8 Agosti mwaka wa 2018 watu 96,136 wamepatiwa chanjo nchini DRC.

Ebola, kwa mara ya kwanza ililipuka mwaka 1976.

Virusi vya Ebola viliennea Afrika Magharibi mnamo Desemba 2013.

Mwaka 2014-2017 nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone, watu elfu 30 waliambukizwa na zaidi ya watu 11,000 walikufa.

Wataalamu wanasema ipo haja ya mataifa yaliyo kwenye hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola kuwekeza zaidi kwenye mikakati ya dharura ya kupambana na ugonjwa huo.

Shirika la afya duniani hata hivyo linasikitishwa kuwa hadi leo fedha zinazowekezwa kupambana na ugonjwa huo ni kidogo mno.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.