SUDANIKUSINI-SIASA-USALAMA
Mvutano waibuka kuhusu uundwaji wa serikali Sudani Kusini
Chama cha South Sudan National Democratic Movement nchini Sudan Kusini, kimeunga mkono wito wa kiongozi wa upinzani Riek Machier, kuahirishwa kwa uundwaji wa serikali ya mpito kwa miezi kadhaa.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
NDM kinasema bado kuna changamoto ya kijeshi na suala la mipaka, mambo ambayo hajapewa ufumbuzi.
Machar ambaye anaishi jijini Khartoum na anayetarajiwa kuwa Makamu wa kwanza wa rais amesema hatorejea Juba, kufanikisha uundwaji wa serikali hiyo mwezi Mei, kwa sababu za kiusalama.
Hata hivyo, rais Kiir amesisitiza kuwa uudwaji wa serikali hiyo utaendelea kama ilivyopangwa.