Pata taarifa kuu
Mali - Usala

Kambi ya UN kaskazini mwa Mali yashambuliwa

Wapiganaji wanaodaiwa kuwa ni kutoka makundi ya kiislamu wameshambulia kambi ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kaskazini mwa nchi ya Mali kwenye mji wa Kidal, ambapo watu kadhaa wameripotiwa kufa na wengine kujeruhiwa, amesema msemaji wa kundi la vuguvugu la Azawadi.

Askari wa Minusma wakipiga doria katika mji wa Kidal, Julai 23, 2015.
Askari wa Minusma wakipiga doria katika mji wa Kidal, Julai 23, 2015. REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Tume ya MINUSMA nchini humo bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu idadi kamili ya watu waliouawa, ingawa msemaji wa tume hiyo, amethibitisha watu kadhaa kupoteza maisha kwenye shambulio hilo lililotekelezwa majira ya saa kumi na mbili asubuhi ya leo.

Kambi hiyo ya walinda amani kwenye mji wa Kidal, ilifunguliwa kwa lengo la kuimarisha usalama kwenye eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, ambalo linaendelea kushuhudia matukoo ya hapa na pale ya wapiganaji wa kiislamu.

Hayo yanajiri wakati kukiwa na taarifa za mauaji ya wanajeshi 3 wa Mali walioanguka katika mtego wa wapiganaji wa kijihadi katika jimbo la Timbuktu kaskazini Magharibi mwa Mali, duru za kijeshi zimethibitisha.

Afisaa mmoja wa jeshi la Mali katika jimbo la Timbuktu ameliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba wenzao watatu wamepoteza maisha baada ya gari lao kuanguka katika mtego wa wapiganaji wa kijihadi katika eneo kati ya Timbuktu na Goundam. Taarifa hii imethibitishwa na kiongozi mmoja kwenye wizara ya ulinzi nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.