Pata taarifa kuu
CAR-UN-UBAKAJI

CAR: tuhuma mpya za unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya MINUSCA

Mara baada ya kukabiliwa na kashfa ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto inayowashirikisha askari wa Ufaransa, Umoja wa Mataifa, mara kwa mara unatuhumiwa kukaa kimya au kupuuzia unyanyasaji wa kijinsia unaovikabili vikosi vyake.

Haijulikani ni askari wa ngapi wa MINUSCA walioshiriki katika kashafa hiyo na ni kutoka nchini gani.
Haijulikani ni askari wa ngapi wa MINUSCA walioshiriki katika kashafa hiyo na ni kutoka nchini gani. © MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumanne hii katika taarifa yake, Umoja wa Mataifa umesema umeanzisha uchunguzi kuhusu kashfa mpya ya unyanyasaji wa kijinsi dhidi ya askari wake wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Waathirika mpaka sasa ni watoto.

Kwa sasa, Umoja wa Mataifa umechukua uamzi. Ili kuonyesha kwamba umejifunza kuhusu kashfa zilizovikabili vikosi vyake siku za nyuma, Umoja wa Mataifa umeamua kutangaza hadharani mashtaka haya mapya. Wasichana wanne, wanaoshukiwa kutendewa maovu hayo walihohojiwa na wapelelezi wa Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto UNICEF mjini Bangui, na sasa wasichana hao wanapata tangu wakati huo huduma ya kisaikolojia, imesema taarifa hiyo.

Haijulikani ni askari wa ngapi walioshiriki katika kashafa hiyo na ni kutoka nchini gani. Kinachojulikana tu ni kwamba askari hao ni kutoka nchi tatu tofauti. Nchi ambazo Umoja wa Mataifa unasema uliziomba kuendesha uchunguzi wao wenyewe na uwezekano wa kuchukua vikwazo.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) umeahidi kufanya kinachowezeka ili kutekeleza sera yake ya "kutosamehe yeyote". Mkuu wa Ujumbe huo, jenerali Parfait Onanga-Anyanga, pia ameahadi kuimarisha hatua za kuzuia maovu hayo yasirudi kutendeka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.