Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-USALAMA

Burundi: Baraza la Usalama la kitaifa lapinga uamzi wa AU

Nchini Burundi, Baraza la Usalama la kitaifa limefutilia mbali uamuzi wa Umoja wa Afrika wa kutuma kikosi cha askari 5,000 nchini humo. Baraza hilo, linaloundwa na vigogo katika serikali ya Burundi, ikiwa ni pamoja na rais Nkurunziza mwenyewe na viongozi kadhaa wa Idara mbalimbali zinazohusiana na sekta ya usalama, lilikutana Jumatatu wiki hii.

Mwili wa mtu aliyeuawa wilayani Cibitoke, kitovu cha maandamano mjini Bujumbura, Desemba 9, 2015.
Mwili wa mtu aliyeuawa wilayani Cibitoke, kitovu cha maandamano mjini Bujumbura, Desemba 9, 2015. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Usalama la kitaifa nchini Burundi limepinga uamuzi wa kutumwa kwa kikosi cha Umoja wa Afrika katika ardhi yake, uamzi ambao unakwenda sambamba na siku ya mwisho ya muda uliyotolewa Ijumaa na Umoja wa Afrika.

Jumanne hii asubuhi, Waziri wa Usalama wa raia ambaye amesoma taarifa katika kipengele chake cha 8 inayosema kuwa inafutilia mbali uamuzi wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika wa kutuma kikosi cha askari wa Afrika cha kulinda amani nchini Burundi. "Tishio la mauaji ya kimbari ambalo ni moja ya madai ya kutumwa kikosi hicho ni hoja isiyokuwa na msingi", kwa mujibu wa Baraza la Usalama la kitaifa. "Hoja ya kukamilisha mapinduzi yaliyoshindwa Mei 13, 2015 ".

Kwa mujibu wa Baraza hilo, "Burundi ni moja ya nchi za Afrika zinazochangia askari kwa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa", hiyo ikiwa ni moja ya sababu ya Burundi kuwa na uwezo wa kulinda usalama wa raia wake.

"Hata hivyo Umoja wa Afrika bado unahitaji askari wengine kutoka Burundi kwa kulinda usalama katika nchi mbalimbali barani Afrika", taarifa ya Braza la Usalama la kitaifa imebainisha.

Msimamo huu ni sawa na ule Baraza mbili za Bunge na Seneti zilitoa Jumatatu wiki hii katika mkutano uliowashirikisha pamoja Wabunge na Maseneta, ikiwa ni pamoja na sawa na msimamo uliotolewa na Naibu msemaji wa rais mwishoni mwa juma lililopita kwenye Idhaa ya Kifaransa ya RFI.

Ukosefu wa usalama ni dhahiri nchini Burundi kwa mujibu wa FRODEBU Nyakuri

"Hili ni Bunge lililochaguliwa kinyume cha sheria. Zote hizi, ni fikra potovu za serikali na chama tawala cha CNDD-FDD", amesema Jean Minani, kiongozi wa chama cha upinzani cha FRODEBU Nyakuri, ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni. Mpinzani huyu anaongeza kuwa ukosefu wa usalama ni dhahiri nchini Burundi, mauaji ya kikatili na mauaji kwa watu wanaokamatwa na maafisa wa serikali, yanaonyesha wazi kuwa kuna ukosefu wa usalama.

Mwanachama mwingine wa upinzani anasema kuwa kuna haja ya kuonyesha msimamo katika shughuli za kulinda amani katika jumuiya ya kimataifa. "unaua raia wako, je unapaswa kuendelea kushiriki katika shughuli za kusimamia amani duniani? " mpinzani mwengine ameuliza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.