Pata taarifa kuu
BURUNDI-UN-USALAMA

UN yatoa picha inayotisha kuhusu hali Burundi

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema anatiwa wasiwasi na mdororo wa usalama na vurugu ambavyo viligharimu maisha ya zaidi ya watu 90 Ijumaa Desemba 11, na kubaini kwamba Burundi sasa imepiga hatua moja mbele kuelekea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Askari akipiga doria katika makaburi mjini Bujumbura, wakati wa mazishi ya Willy Nzitonda, mtoto wa mwanaharakati wa haki za binadamu Pierre Claver Mbonimpa, Novemba 10, 2015.
Askari akipiga doria katika makaburi mjini Bujumbura, wakati wa mazishi ya Willy Nzitonda, mtoto wa mwanaharakati wa haki za binadamu Pierre Claver Mbonimpa, Novemba 10, 2015. © AFP PHOTO / LANDRY NSHIMIYE
Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa New York, mashirika mawili yanayohusika na misaada ya kibinadamu, OCHA na UNICEF, yametoa tahadhari. Ukosefu wa fedha unaweza kuchangia kuongezeka kwa vurugu.

Hii ni hali ya kutisha ambayo maafisa wawili wa Umoja wa Mataifa wameelezea waliporudi kutoka ziara yao nchini Burundi. Watu 700,000 wanakosa chakula, sawa na 36% ya raia. 80% ya raia wa Burundi wanaishi katika hali ya umaskini. Lakini hasa, zaidi ya euro milioni 29 bado zinakosa katika hazina ya mashirika ya kibinadamu ambayo yanaendesha harakati zao nchini Burundi.

"Kama hakuna msaada wa maendeleo au msaada wa kibinadamu uliyowekwa katika bajeti ya misaada, rasilimali zilizopo hazitoshi kugharamia gharama za huduma zinazohitajika kwa raia", mmoja wa maofisa hao wawili ameonya.

Matokeo: Huduma za Afya tayari zimeanza kukabiliana na uhaba wa dawa na huduma zilizokua zikitolewa kwa bure kwa watoto walio na umri ulio chini ya miaka 5 na kwa wanawake wajawazito zimesimamishwa.

Jukumu la Umoja wa Mataifa matatani

Mjini New York, Umoja wa Mataifa unanyooshewa kidole cha lawama kwa kutowajibika kutatua mgogoro nchini Burundi. Tathmini ambayo mkurugenzi wa shughuli za kibinadamu, John Ging, amekataa kufanya.

"Katika kile Umoja wa Mataifa unafanya katika nyanja ya kisiasa, hatuwezi kujitosa juu ya suala hilo", John Ging amesema. "Kinachotutia wasiwasi, ni kuhakikisha kwamba sisi, mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, na washirika wetu ambayo ni mashirika yasio ya kiserikali yanafanya kile tunachotakiwa kufanya. "

Lakini wito umeendelea kutolewa na hasa kuanzisha operesheni za kulinda amani ambazo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikua halijakubaliana hadi sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.