Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-MAUAJI-USALAMA

AU mbioni kuwatuma wanajeshi wake Burundi

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limepitisha azimio la kuwatuma wanajeshi wake 5000 nchini Burundi ili kuzuia mlipuko wa mauaji ya kimbari nchini humo, ambayo yanahofiwa kutokea wakati wowote.

Maiti zikiokotwa katika mitaa ya Bujumbura asubuhi ya Desemba 12, 2015.
Maiti zikiokotwa katika mitaa ya Bujumbura asubuhi ya Desemba 12, 2015. © REUTERS/Jean Pierre Aime HarerimanaTEMPLATE OUT
Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo unachukuliwa wiki moja baada ya mauaji ya zaidi ya watu 90 katika wilaya ambayo ni kitovu cha maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza. Vikosi vya usalama na ulinzi pamoja na wanamgambo wa chama tawala cha CNDD-FDD wananyooshewa kidole kutekeleza kwa maksudi mauaji hayo.

Mauaji hayo yalitokea baada ya zaidi ya saa 4 ya mapigano katika kambi tatu za jeshi mjini Bujumbura.

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limetoa siku 4 tangu Alhamisi hii kwa serikali ya Burudi itafakari azimio hilo, na iweze kutoa jibu sahihi, la sivyo Baraza hilo linasema litatumia nguvu kulingana na uwezo linalopewa na Katiba yake.

Machafuko nchini Burundi yamesababisha zaidi ya watu 400 kupoteza maisha kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu na za wafungwa APRODH, na wengine zaidi ya 200,000 kuyahama makaazi yao.

Wakati huo huo Baraza la Umoja wa Ulaya limesema kuwa hali inayojiri wakati huu nchini Burundi inatisha, na kuomba Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka ili kuzuia wimbi la mauaji ya kimbari linalohofiwa kutokea.

Hata hivyo miili ya watu wanaouawa imekua ikiokotwa kila kukicha katika mitaa ya Bujumbura na katika baadhi ya maeneo mikoani.

Tume ya haki za binadamu kwenye Umoja wa Ulaya imetoa azimio kuhusu hali ya Usalama nchini Burundi na kuamuru kuanzishwa kwa mazungumzo na kutumwa kwa wachunguzi wa haki za binadamu nchini humo baada ya mauaji ya hivi karibuni yaliogharimu maisha ya watu zaidi ya 90 hivi karibuni.

Tume hiyo pia inataka mahakama kuu ya uhalifu wa kivita ya ICC kufanya uchunguzi kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu, na kuomba Umoja wa Ulaya kuiwekea vikwazo serikali ya Burundi, na kuzuia misaada kufika nchini humo.

Mbunge wa bunge la Ulaya kutoka chama cha Kisociliasti nchini Uturuki Maria Arena anasisitiza kwamba inafaa kuhakikisha nchi hiyo inaepukana na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu mzozo huo unaweza kusambaa hadi katika nchi za ukanda wa maziwa makuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.