Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAANDAMANO-USALAMA-SIASA

Hali ya kisiasa na usalama yaendelea kuwa tete Burundi

Hali imeendelea kuwa tete jijini Bujumbura, nchini Burundi wakati huu mashirika ya kiraia yakitoa wito wa kuendelea na maandamano.

Wanajeshi wa Burundi wakipiga doria katika mji mkuu Bujumbura, Mei 29 mwaka 2015.
Wanajeshi wa Burundi wakipiga doria katika mji mkuu Bujumbura, Mei 29 mwaka 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi nchini humo Pierre Claver Ndayicariye amekiri kujiuzulu kwa wajumbe wawili wa tume ya uchaguzi.

Ukosefu wa habari sahihi nchini Burundi imekuwa sababu za kuwatia hofu wananchi wa taifa hilo ambapo wakati huu kumekuwa na uvumi wa kila aina.

Jumapili Mei 31 wakati Pierre Nkurunziza akiwa katika shughuli za kampeni ya Uchaguzi mkoani Ngozi alionya kuhusu kutokea kwa jaribio jingine la mapinduzi na kuwahakikishia wafuasi wake kwamba hakuna jaribio lolote linaloweza kufaanikiwa.

Hayo yakijiri, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Burundi (Céni) Pierre Claver Ndayicariye amekiri kuwa wajumbe wawili kati ya watano wanaounda tume ya uchaguzi wamejiuzulu na kuwakilisha barua zao Jumatau jioni wiki hii.

Wajumbe hao wamesema hatuwa ya kujiuzulu ni kutokana na maandalizi ya uchaguzi ambao wanaona kwamba hauwezi kuwa huru na haki kulingana na mazingira yaliopo wakati huu.

Umoja wa mataifa umesema hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu imesababisha watu zaidi ya elfu sabini kukimbilia nchini Rwanda, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo kitita cha dola za marekani milioni 15 zimetolewa kwa ajli ya msaada kwa wakimbizi hao.

Kulikuwa na utulivu Jumatatu wiki hii katika maeno kadhaa ya jiji la Bujumbura baada ya kikao cha marais wa jumuiya ya Afrika mashariki jijini Dar es Salaam, lakini wito umetolewa tena hii leo wa kuendelea na harakati za maandamao kupinga muhula wa 3 wa rais Pierre Nkurunziza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.