Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC

Muafaka kuhusu amani kujadiliwa Colombia

Nchini Colombia, baada ya kura ya maoni kukataa kwa 50.2% makubaliano ya amani na kundi la waasi la FARC, Rais Juan Manuel Santos ameitisha vyama vya siasa kuanza mazungumzo na upinzani, ikiwa ni pamoja na chama cha rais wa zamani Alvaro Uribe.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha waalimu wakiandamanambele ya jengo la Bunge la Colombia, Bogota, Oktoba 3, 2016.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha waalimu wakiandamanambele ya jengo la Bunge la Colombia, Bogota, Oktoba 3, 2016. REUTERS/John Vizcaino
Matangazo ya kibiashara

Rais Alvaro Uribe aliongoza kampeni ya kukataa makubaliano na kundi la waasi la FARC, akisemaanataka waasi waliofanya uhalifu kuchukuliwa hatua ya kuwekwa gerezani na baadhi ya viongozi wa kundi la waasi la FARC kufungiwa kujihusisha na siasa.

WAkati huo huo, wanafunzi wa Chuo Kikuu waliandamana Jumatatu hii mchana katikati mwa mji wa Bogota dhidi ya Rais wa zamani Alvaro Uribe.

Walikuwa takriban wanafunzi mia mbili wa Chuo Kikuu cha waalimu ambao waliandamana katika mtaa wa Carrera 7, mtaa unaopita katia mji mkuu wa Colombia, Bogota, kuanzia kaskazini hadi kusini. Wanafunzi hao waliandamana wakiwa na mabango yaliyoandikwa "Ndiyo kwa amani, hapana kwa vita". Walikua wakiomba serikali kutosahau kina cha makubaliano ya amani na kundi la waasi la FARC.

Waliandamana wakionyesha hasira yao dhidi ya chama cha upinzani cha rais wa zamani Alvaro Uribe, ambacho kama walivyosema wao wenyewe, kiliendesha kampeni ya chuki ambayo imesababisha ushindi wa "hapana" katika kura ya maoni ya Jumapili.

Awamu mpya ya mazungumzo na FARC

Jumatatu hii, Rais Juan Manuel Santos ameitisha vyama vya siasa ambavyo vilipitisha kuundwa kwa Kamati ya kitaifa ya mazungumzo, mazungumzo ambayo upinzani umealikwa kushiriki.

Rais wa Colombia Pia ametangaza awamu mpya ya mazungumzo na kundi la waasi la FARC. "Ninamuomba Humberto de la Calle, ambaye ninathibitisha kama mpatanishi mkuu (...), kuanzisha mazungumzo ambayo yataturuhusu kushughulikia masuala yote muhimu ili kufikia makubaliano na ndoto ya kukomesha vita na kundi la waasi la FARC," Rais Juan Manuel Santos amesema Jumatatu hii jioni wakati wa hotuba kwenye televisheni.

Mapema Jumatatu wiki hii, kiongozi kundi la waasi la FARC alisema yuko tayari "kurekebisha" mkataba wa amani uliyokataliwa na kura ya maoni ya Jumapili, huku akihakikisha kwamba waasi watasalia kuwa wa "wakweli kwa makubaliano yaliyoafikiwa" .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.