Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC

Serikali ya Colombia na waasi wa FARC wasaini mkataba wa amani wa kihistoria

Jumatatu hii, Septemba 26 serikali ya Colombia na waasi wa kundi la FARC walisaini mkataba wa amani. Sherehe hizo zilifanyika katika mji wa Cartagena, kaskazini mwa nchi. Makubaliano hayo yanamaliza zaidi ya nusu karne ya vita vya vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu, na wengine kulazimika kuyahama makazi yao.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos (katikati), akiwa na kalamu iliyotengenezwa kwa risasi, na kiongozi wa FARC (kulia) wakati wa kusainiwa kwa mkataba wa amani, Septemba 26, 2016 katika mji wa Cartagena.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos (katikati), akiwa na kalamu iliyotengenezwa kwa risasi, na kiongozi wa FARC (kulia) wakati wa kusainiwa kwa mkataba wa amani, Septemba 26, 2016 katika mji wa Cartagena. REUTERS/John Vizcaino
Matangazo ya kibiashara

Colombia sasa imeingia katika ukurasa mpya wa kihistoria, Jumatatu hii, Septemba 26, 2016, pamoja na sherehe ya kutia saini mkataba wa amani kati ya serikali na waasi wa kundi la FARC katika mji wa Cartagena.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos na kiongozi wa kundi la waasi wa FARC wametia saini mkataba wa amani kumaliza miongo mitano ya uhasama wa kivita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Katika hafla iliyofanyika huko mjini Cartagena wametumia kalamu iliyotengenezwa na risasi kusaini mkataba huo, na kisha kwa mara ya kwanza wakapeana mikono wakiwa ardhi ya Colombia.

Watu 2,500 wamealikwa kuhudhuria sherehe hiyo ya kihistoria ambayo inatamatisha zaidi ya miaka 50 ya vita na kundi kubwa la watu wenye silaha katika bara la Amerika. Mgogoro ambao amesababidha vifo vya watu 220 000, huku watu 40,000 wakitoweka na wakimbizi wa ndani zaidi ya milioni 7 nchini kote.

Kiongozi wa kundi hilo la FARC kamanda Rodrigo Londono, anayejulikana vyema kwa jina Timochenko, amewaomba msamaha waathiriwa wote wa vita hivyo.
Waliohudhuria hafla hiyo walikuwa wamevalia mavazi ta rangi nyeupe, kuashiria amani.

Naye Rais Juan Manuel Santos amesema: "Colombia inasherehekea, ulimwengu unasherehekea kwa sasa kuna vita vimemalizika duniani."

Tutatimiza malengo yote, tutazidi nguvu changamoto zote na kugeuza nchi hii kuwa taifa ambalo tumekuwa tukitaka liwe, taifa la amani."

Ilibidi miaka minne ya mazungumzo kati ya serikali na waasi wa kundi la FARC ili kuhitimisha makubaliano hayo. Mikataba ambayo haiungwi mkono kwa kauli moja, wapinzani wanakosoa ahadi za serikali kwa waasi na dhamana haitoshi. "Bora amani isio kamili kuliko vita kamili," amejibu Rais wa Colombia Juan Manuel Santos.

Siku ya Ijumaa, kundi la waasi la FARC lilitangaza kuridhia mikataba isiyopingwa, katika mkutano wake wa kumi. "Vita vimemalizika," amesema kiongozi wa ujumbe wa kundi la waasi la FARC katika mazungumzo Ivan Marquez.

Mikataba ilisainiwa katika mji wa Havana Agosti 24 kati ya pande mbili zilizokua zikishiriki mazungumzo. Lakini kulikua kunahitajika tendo la kihistoria kwenye ardhi ya Colombia ili kuidhinisha makubaliano hayo.

Marais kumi na tano kutoa nchi mbalimbali, Mawaziri wa Mambo ya Nje na viongozi wa ngazi za juu, ikiwa ni pamoja na Rais wa Cuba Raul Castro,mwenyeji wa mazungumzo ya amani, Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani John Kerry na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, wamehudhuria sherehe hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.