Pata taarifa kuu
NIGER-CHAD-UINGEREZA-USHIRIKIANO

Uingereza kufungua ubalozi Chad na Niger

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, ambaye anafanya ziara ya kiserikali barani Afrika, amesema Jumatano wiki hii kwamba siku za usoni kutafunguliwa balozi mbili za Uingereza nchini Chad na Niger ili kupambana na "kudorora kwa usalama" katika "moja ya maeneo tete" barani Afrika.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, yuko ziarani barani Afrika.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, yuko ziarani barani Afrika. REUTERS/Toby Melvillle
Matangazo ya kibiashara

Bi May, ambaye anazuru Nigeria leo Jumatano baada ya Afrika Kusini Jumanne wiki hii, pia ametangaza kuongeza idadi ya wafanyakazi katika ubalozi wa Uingereza nchini Mali.

"Katika moja ya maeneo tete barani Afrika, tunaimarisha uungwaji wetu mkono kwa juhudi zinazofanywa na nchi za Afrika kwa kupambana dhidi ya mdororo wa usalama na migogoro," amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Upanuzi huu wa mtandao kidiplomasia inapaswa kusaidia "kupunguza vitisho uwezo wa usalama wa Uingereza na Ulaya," wizara alisema.

Mpaka sasa Uingereza imekua tu na "ofisi" nchini Chad na Niger, lakini mambo mengi yamekua yakitumwa kwenye balozi zake huko Yaounde, nchini Cameroon, na Bamako, nchini Mali.

Chad na Niger, kama nchi jirani kadhaa zinakabiliwa na mdororo wa usalama kutokanana mashambulizi ya kila mara ya makundi ya wanamgambo wa Kiislamu ikiwa ni pamoja na Boko Haram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.