Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-SIASA

Baraza la Walei latishia kuchukua hatua mpya dhidi ya serikali

Kamati ya Baraza la Walei ya Kanisa katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, (CLC) imedai kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi CENI imekuwa ikishawishika na upande wa rais Joseph Kabila kwa kuhakikisha mashine za kielektroliki zinatumiwa wakati wa uchaguzi mkuu wa desemba 23 mwaka huu nchini humo.

Maakofu wa Kanisa Katoliki DRC, (CENCO).
Maakofu wa Kanisa Katoliki DRC, (CENCO). Photo MONUSCO/ John Bompengo
Matangazo ya kibiashara

Mbali na swala hilo, kamati hiyo imesema ina ushahidi tosha kuwa rais Joseph Kabila yuko tayari kuwania muhula wa tatu kwenye uchaguzi huo, na hiyo kinyume cha sheria.

Kufwatia hali hiyo, Kamati ya baraza la walei ya kanisa katoliki imeitisha mgomo wa kitaifa, pamoja na maandamano kwa tarehe tofauti kuanzia tarehe 09 mwezi ujao, kama anavyoeleza katibu mtendaji wa kamati hiyo, Professa Isidore Ndayiwell,

Hayo yanajiri wakati ambapo mshauri wa masuala ya kidiplomasia nchini DRC amesema ziara ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo haitakuwa na umuhimu kwa wakati huu taifa hilo likijiandaa na uchaguzi wa badaae Disemba mwaka huu.

Kwa kujibu kuhusu haja ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuzuru DRC na rias wa Umoja wa Afrika, tunafikiri kuwa haitakuwa na umuhimu kwa wakati huu DRC ikijiandaa na uchaguzi wa badaae Desemba mwaka huu ", amesema Kikaya Bin Karubi, mshauri wa masuala ya kidiplomasia wa Joseph Kabila.

"Hakuna tarehe iliyotangazwa, kwa sasa hakuna kitu kilichopangwa" kwa kutarajia ziara ya Antonio Guterres nchini DRC, amesema kwa upande wake Florence Marchal, msemaji wa Monusco, akiliambia shirika la habari la AFP.

Mwishoni mwa mwezi Januari, rais Kabila alishutumu ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) akitaka kuondoka nchini ifikapo mwaka 2020.

Wanasiasa nchini DRC wamekua wakihitilafiana kuhusu Kabila kuwania au la katika uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.