Pata taarifa kuu
DRC-ADF

DRC: Hofu yaenea kwenye mji wa Beni baada ya raia 10 kuuawa

Raia 10 na mpiganaji mmoja wa kundi la waasi wa Uganda wamekufa wakati wanajeshi wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walipokabiliana na waasi kwenye mji wa Beni mashariki mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa Serikali ya DRC, FARDC wakifanya doria kwenye mji wa Beni.
Wanajeshi wa Serikali ya DRC, FARDC wakifanya doria kwenye mji wa Beni. ALAIN WANDIMOYI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yalitokea siku ya Jumanne jioni wakati waasi waliposhambulia kambi za jeshi kwenye maeneo ya Beni, jimboni Kivu Kaskazini, amesema msemaji wa jeshi Mak Hazukay.

"Tumeorodhesha raia 10 mpaka sasa," amesema Hazukay.

Mpiganaji mmoja wa kundi la waasi wa Uganda ADF pia aliuawa, alisema msemaji wa jeshi aliyethibitisha operesheni za jeshi kuendelea.

Michel Kakule ambaye ni daktari kwenye hospitali ya Beni aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa baadhi ya majeruhi walikuwa na majeraha ya risasi na wengine walikuwa na majeraha ya kukatwa na mapanga.

mapigano haya yalitokea baada ya baadhi ya raia kufunga barabara za kuingia kwenye mji huo kutokana na mauaji ya raia 10 alisema Gilbert Kambale ambaye anafanya kazi na shirika moja la kiraia.

Tangu mwezi Januari majeshi ya DRC yamekuwa yakikabiliana na waasi wa Uganada katika operesheni inayoendelea mashariki mwa nchi hiyo lakini mpaka sasa hawajafanikiwa kuzima mauaji yanayofanywa na kundi hili.

Jeshi la DRC linasema wapiganaji wa ADF wamebadilisha mbinu za kushambulia raia ambapo wakikabiliana upande mmoja wa najeshi wanahamia upande mwingine kutekeleza mauaji.

Kundi hili la kiislamu ambalo liliundwa na waislamu wenye msimamo mkali kuipinga Serikali ya rais Yoweri Museveni, limekuwa na makazi yake mashariki mwa DRC jimboni Kivu kaskazini tangu mwaka 1995 ambako linalaumiwa kwa mauaji ya mamia ya raia.

Kundi hili pia linalaumiwa kwa kuhusika katika shambulio lililoua walinda amani 15 wa umoja wa Mataifa kutoka Tanzania katika mji wa Beni mwezi Desemba mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.