Pata taarifa kuu
DRC--M23-USALAMA

Waasi wa zamani wa M23 waingia DRC

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokarsi ya Congo imetangaza kwamba wapiganaji wa zamani yumkini 200 wa kundi la zamani la waasi la M23 wameingia nchini DRC kutoka nchi jirani ya Uganda.

wapiganaji wa kundi la zamani la M23, Februari 2014.
wapiganaji wa kundi la zamani la M23, Februari 2014. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Serikali Lambert Mende ameilaumu Uganda kwa kuwaruhusu watu hao kuvuka mpaka na kunigia nchini DRC bila hata hivyo kfahamisha viongozi husika.

Bw Mende amesema kuwa jeshi la Congo limekabiliana na watu hao. Waasi wazamani wa M23 lilikua likiundwa na wapiganaji wengi kutoka jamii ya Watutsi kutoka DR Congo na baadhi wapiganaji kutoka makabila mengine mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kundi la zamani la waasi la M23 lilishindwa na jeshi la Congo mwaka 2013, baada ya kutimuliwa kwenye milima iliyo katibu na mji wa Goma na kukimbilia nchini Uganda.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekua ikiendesha harakati za kuwapokonya silaha waasi hao lakini harakati hizo zilisitishwa.

Hadi sasa swaasi wa zamani wa kundi la zamani la M23 wanaishi katika kambi za wakimbizi nchini Uganda na Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.