Pata taarifa kuu
MALI-SANOGO-SHERIA

Kesi ya Amadou Sanogo yasitishwa hadi Desemba 2

Kesi ya Amadou Sanogo, kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Mali anayeshtakiwa kwa "mauaji na kula njama katika mauaji" ya askariimeahirishwa hadi Desemba 2 kwa ombi la upande wa utetezi.

Amadou Sanogo akanusha kuhusika kwake moja kwa moja katika mauaji ya askari zaid ya ishirini nchini Mali.
Amadou Sanogo akanusha kuhusika kwake moja kwa moja katika mauaji ya askari zaid ya ishirini nchini Mali. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Afisa huyo wa jeshi amekua akisikilizwa tangu Jumatano Novemba 30, na washitakiwa wenzane 16 kwa "utekaji nyara na mauaji, kula njama za utekaji nyara na mauaji" ya askari ambao miili yao ilikutwa katika kaburi la pamoja mwaka 2013. Katika kesi hiyo inayojulikana kama "Berets Rouge », Amadou Sanogo anakabiliwa na adhabu ya kifo lakini alisema wa ufunguzi wa kesi yake kwamba "hajakata tamaa ".

Awali kesi hii ilipangwa kusikilizwa kwenye mahakama ya Sikasso, kilomita 370 kusini-mashariki mwa mji wa Bamako, hatimaye kesi hiyo ilisikilizwa katika ukumbi unaoweza kupokea watu wengi. Sehemu ambapo kesi hii ingelisikilizwa ilionekana ni finyo. "Kesi hii itakua na muda wa kutosha ili kuidhihirisha ukweli," alisema Mwendesha Mashitaka Mkuu Mamadou Lamine Coulibaly, mwanzoni mwa kesi hii mbele ya umati wa watu walio kuwa wamekuja kusikiliza.

Sanogo anakanusha kuwa anahusika moja kwa moja

Wakipinga mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Machi 2012 yakiongozwa na Amadou Sanogo, afisa huyo wajeshi, ambaye alimpindua rais Amadou Toumani Touré, askari waliouawa walijaribu bila mafanikio kuzuia mapinduzi hayo mwezi mmoja baadaye kabla ya kutimuliwa na kikosi kiliyoendesha mapinduzi hayo. Miili ya askari ishirini iligunduliwa baadaye mwezi Desemba 2013 katika kaburi la pamoja katika mji wa Diago, karibu na mji wa Kati, ambapo kikosi cha askari wa jenerali Sanogo kilikua kilipiga kambi.

Hata hivuo madou Sanogo alikanusha kuhusika kwake moja kwa moja katika mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.